The House of Favourite Newspapers

Alichokizungumza Julius Mtatiro Baada ya CUF Kuvamiwa na Watu Wasiojulikana

0

KUFUATIA Kundi la watu wasiofahamika waliokuwa wamevalia kininja wakiwa na MAPANGA na BASTOLA moja kuvamia mkutano wa Chama Cha Wananchi (CUF) na kudaiwa kuwapiga viongozi na wanahabari.

Katika Mkutano huo, Mwenyekiti wa CUF wilaya ya Kinondoni na Mjumbe wa Baraza Kuu Mhe. Juma Mkumbi alikuwa anazungumza na Vyombo vya Habari katika Hoteli ya Vina iliyoko kata ya Mabibo, Dar ambapo baada ya tukio hilo la kutisha, wananchi na wafuasi wa CUF waliokuwa eneo la tukio walitaharuki.

Kufuatia tukio hilo, Mtatiro ameyasema haya kupitia ukurasa wake wa Instagram.

  • KUHUSU KUNDI LA LIPUMBA KUVAMIA VIONGOZI WA CHAMA… Wengi mmeniuliza kuhusu viongozi wa CUF kuvamiwa, ni kweli. Leo Mwenyekiti wa CUF wilaya ya Kinondoni na Mjumbe wa Baraza Kuu Mhe. Juma Mkumbi alikuwa anazungumza na Vyombo vya Habari katika Hoteli ya Vina iliyoko kata ya Mabibo, Dar.
    Ghafla mkutano wake ukavamiwa na kundi la Lipumba liitwalo MUNGIKI. Wavamizi hao walivalia kininja wakiwa na MAPANGA na BASTOLA moja. Wavamizi wakaanza kuwapiga viongozi na wanahabari wakiwatuhumu kuwa kwa nini hawamuungi mkono Lipumba.Waandishi Na kadhaa na viongozi kadhaa wamejeruhiwa, kuporwa simu zao, kamera, vitendea kazi, fedha n.k. Wananchi wa Mabibo waliposikia mayowe na kelele za kuomba msaada walipandisha ghorofani (kwenye PRESS) ili kutoa msaada.

    Kuona wananchi wanakuja kwa wingi, kundi la MUNGIKI likaanza kushuka mbio kuelekea kwenye magari mawili waliyokuja nayo. Baadhi ya Mungiki hawakuyafikia magari na wakazidiwa nguvu na wananchi.

    Huyu aliyeko pichani ni Mungiki mmojawapo aliyedhibitiwa na wananchi wenye hasira kali, baada ya kumkimbiza na kumkamatia mitaanu ambapo inasemekana amevunjwa kisigino na mfupa umetokea nje (So sorry and sad). Huyu wa pichani pia ni mmoja wa walinzi wa Lipumba na mara nyingi huwa pamoja na Lipumba. Bahati nzuri, vyombo vya habari vimemhoji mbele ya wananchi na amekiri kuwa UVAMIZI walioufanya umetokana na maagizo ya LIPUMBA.

    Chama chetu kimekwishatoa taarifa rasmi kwenye vyombo vya habari (unaweza kuisoma kwenye ukurasa wangu wa FB). Tumestushwa na kusikitishwa sana na tukio hili baya na la aibu kabisa.

    Chama chetu kimetoa pole kwa waandishi wa habari na viongozi wa majukwaa ya waandishi na kimelitaka jeshi la Polisi lichukue hatua za haraka dhidi ya LIPUMBA na genge lake lijiitalo MUNGIKI.

    #Mtatiro J

  • annayesayaDuuu inasikitisha hapo lipumba hayupo wewe unavunjwa kiuno nyie vijana acheni siasa chafu on a sasa umepata chai ya kutosha
  • jr.huseniNae process uchwara ama kweli kisicho riziki hakiliki
  • mmahmoudjabirMasikini roho yake

Leave A Reply