The House of Favourite Newspapers

Aliens ndani ya sayari ya mars?

0

Aliens — extraterrestrialsILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:
Mpenzi msomaji wiki kadhaa niliona ni vyema tukatoka nje ya boksi na kupata simulizi ya viumbe wa ajabu wa Aliens wanaodaiwa kuishi angani. Wiki iliyopita nilieleza namna ambavyo kuna kila dalili kwamba kuna viumbe wengine nje ya dunia tunayoishi ikiaminika kuwa ni hao Aliens. SASA ENDELEA…

Katika kufanya utafiti inaelezwa kwamba wanasayansi waligundua kuwa kuna maisha nje ya Sayari ya Dunia katika Sayari ya Mars. Inaaminika kwamba kuna viumbe wanaishi katika sayari hiyo. Inatajwa kuwa, viumbe wanaoishi katika Sayari ya Mars wameendelea sana kiteknolojia kuliko binadamu. Ufahamu wao ni mkubwa mara nyingi zaidi ya ule wa wanadamu.

Serikali ya Marekani kwa kushirikiana na kituo cha anga cha NASA wanadaiwa kwamba wanafahamu ukweli wa jambo hilo lakini wanauficha kwa binadamu kwa sababu wanazijua wao wenyewe.

Kabla ya jambo hilo, kwa muda mrefu wanasayansi wamekuwa wakitafuta uwezekano wa maisha katika sayari nyingine mbali na dunia.

Kuna imani kuwa kwenye sayari hizo, huenda kuna rasilimali nyingi kwa urahisi kuliko duniani ambako binadamu wameishi maelfu ya miaka hadi sasa.

Wataalam hao wa anga wamekuwa wakifanya utafiti huo kwa muda sasa na moja ya mambo muhimu ambayo wamekuwa wakiyaangalia ni upatikanaji wa maji. Popote maji yanapopatikana, wanaamini maisha yanawezekana. Moja ya sayari ambazo wamekuwa wakiichunguza kwa miaka mingi sasa ni Sayari ya Mars ambayo ni ya nne kutoka kwenye jua. Dunia ni ya tatu.

Inaelezwa kwamba sababu kuu za kuichagua sayari hiyo tofauti na zingine ni kwamba, hali ya hewa inatofautiana kidogo sana na ya dunia.Sayari nyingine kama Mercury na Venus, zipo karibu zaidi na jua na hali ya joto iko juu kiasi kwamba hali ya maisha inaweza kuwa tabu.

Sayari ya Mars ambayo wanasayansi wanaipa jina la Sayari Nyekundu ipo karibu na dunia, hivyo ni rahisi kufika iwapo wanasayansi watathibitisha iwapo maisha yanawezekana huko.

Wanaiita sayari nyekundu kwa sababu eneo kubwa la uso wake ni wa rangi nyekundu, tofauti na nyingine zilizomo kwenye mfumo wetu wa sayari.

Hakuna mwanasayansi ambaye amethubutu kusafiri hadi kwenye sayari hiyo kutokana na ugumu wa kupata vyombo vya kuaminika, vinavyoweza kusafirisha watu kutoka duniani hadi Mars na kurudi salama.

Hata hivyo, hilo siyo tatizo kwa sababu wakibaini mazingira mazuri, utengenezaji wa vyombo hivyo hauwezi kuwapa tabu.Kazi ya uchunguzi imekuwa ikifanywa kwa vyombo maalum ambavyo havina watu lakini vina uwezo wa kuleta mawasiliano duniani.

Pia wanatumia viona mbali katika mchakato huo kuchunguza hali ilivyo kwenye sayari hiyo ambayo kumekuwapo na hisia kwamba huenda waliwahi kuishi viumbe hai mamilioni ya miaka iliyopita lakini baadaye mazingira yakabadilika na kuwa mabaya.

Uchunguzi unaonesha kuwa, Sayari ya Mars ina mabonde mengi ambayo yana kila dalili kuwa awali yalikuwa yanatiririsha maji kama ilivyo mito ya hapa duniani.

Kwa muda mrefu, wanasayansi wamekuwa wakiichukulia sayari hiyo kuwa na mazingira ya jangwa yanayotokana na ukame wa muda mrefu.

Hata hivyo, tafiti za hivi karibuni zilikuja na maelezo kwamba sayari hiyo ina kiwango kikubwa cha maji na mengi yapo mita chache kutoka uso wake.

Mmoja wa wanasayansi wanaochunguza sayari hiyo ni Profesa Jay Melosh wa Chuo Kikuu cha Purdue nchini Marekani. Yeye anasema uchunguzi huo umewapa imani siyo tu kwamba Mars ina maji bali kuna viumbe ambao siyo binadamu na bakteria ambao wanaendelea kuishi humo hadi leo hii.

Ni uchunguzi ambao wanaamini una matumaini tofauti na taarifa za uchunguzi uliopita na kizuri zaidi pia ni kubaini kuwa maji yapo kwa wingi zaidi.
Kwa sababu hiyo, wanaamini kwamba maisha yakianza kwenye Sayari ya Mars, kuna uwezekano pia binadamu wakahamia huko.

Taarifa za uwepo wa maji kwenye sayari hiyo zilitolewa kwenye mkutano wa wanasayansi wanaochunguza anga za mbali, uliofanyika nchini Australia, Juni, mwaka huu.

Moja ya dalili za uwepo wa maji ni vimondo ambavyo vimekuwa vikianguka kwa wingi kwenye uso wa sayari hiyo.

Mtaalam wa Uhandisi na Mambo ya Anga, Profesa Kathleen Howell anasema picha walizopiga maeneo ambayo vimondo vimegonga uso wa Mars, zilionesha dalili kama za mtu aliyetupa jiwe kwenye eneo lenye tope.

Je, nini kitaendelea? Usikose wiki ijayo.

Leave A Reply