The House of Favourite Newspapers

Aliens wahusishwa na chapa ya mnyama siku za mwisho

1

Scary_Movie_Aliens.jpgILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA

Wiki iliyopita nilieleza namna ambavyo kuna kila dalili kwamba viumbe hawa wa ajabu waishio angani wa Aliens wamekuwepo enzi na enzi tangu Agano la Kale. Mbali na Aliens lakini viumbe wasioonekana wapo wengi mno na bado kuna jamii kubwa sana ya virusi ambavyo bado havijagundulika. SASA ENDELEA…

Katika hali kama hiyo, kuna andiko kutoka kwenye Aliens Encounters kuwa viumbe hawa pamoja na vitu vinavyoonekana angani visivyoeleweka almaarufu kwa jina la Ufo ni viumbe wasiojulikana, ambao wanadaiwa kutumiwa na mataifa makubwa kiusalama kwa maelezo kwamba huwapa nguvu ya kujilinda kwa kiwango cha juu.

Kuna habari za kutisha kuwa kwenye Kitabu cha Ufunuo katika Agano Jipya la Biblia inaelezwa kuwa wakati wa mwisho wa dunia kutakuwepo sheria ya kupigwa chapa ya mnyama kwenye paji la uso.

Madai ambayo hayana uthibitisho yanasema kazi hiyo itafanywa na viumbe kutoka sayari nyingine tofauti na Sayari ya Dunia. Viumbe hao si wengine bali ni hawa Aliens.

Hata hivyo, kunapokuwa na habari kama hizi, mwanadamu anapaswa kuwa makini kutoamini kila kinachosemwa au kuandikwa kwenye mitandao kwani mambo mengi duniani yamekuwa yakipotoshwa kwa makusudi ili kukidhi matakwa ya mpotoshaji.

Kwa mfano; wapo watu wanaojua kabisa kwamba Ufo si viumbe bali ni vifaa vilivyotengenezwa na wanasayansi wa Marekani kwa kushirikiana na Aliens lakini imekuwa ikipotoshwa kwa makusudi kuwa ni viumbe wa kutoka sayari nyingine.

Katika hili, Wamarekani hawataki kabisa mataifa mengine wajue uhusiano wao na Aliens kwa sababu viumbe hao wamekuwa wakihusishwa moja kwa moja na utawala wa shetani.

Huko nyuma nilishata-hadharisha kuwa siyo kila kitu unachokutana nacho mitandaoni ni cha kweli. Katika ulimwengu tulionao wa teknolojia mtu yeyote anaweza kujitungia jambo lake kwa fikra na malengo yake kisha akaweka mtandaoni hivyo haima-anishi kwa jambo likishawekwa mtandaoni ni la kweli.

Mfano mzuri ni Sinema za Babylon 5 zenye kuonesha maisha yanavyoendelea huko angani huku wahusika wakuu wakiwa ni Aliens.

Kwa kifupi, Vampires, Aliens, Super Heroes na nyingine ni simulizi za kufikirika huku baadhi ya maandiko ya kisayansi yakijichanganya. Kuna maandiko yanayoeleza kuwa hakuna kiumbe kingine kilichogundulika nje ya sayari hii dunia. Kilichopo ni makisio na fikra kuwa huenda kuna uwezekano wa kuwepo kwa uhai kulingana na hali ya hewa na dalili ya uwepo wa maji.

Video nyingi tunazoziona kutoka Nasa na kwingine juu ya Aliens ni maendeleo tu ya kisayansi ndiyo maana Hollywood, Marekani wameendelea kutengeneza sinema za sampuli hiyo kwa kuwa zina soko kubwa duniani kote pamoja na kwamba zinatisha.

Vyovyote itakavyokuwa, Aliens wawepo au wasiwepo, tukubaliane kwamba binadamu ni kiumbe mwenye akili sana na watu watakaoishi kipindi kijacho cha miaka kadhaa mbele cha ustaarabu, watakuwa na maendeleo ambayo kama utabahatika kuamshwa kutoka usingizi wa kifo utakapokuwa umelala basi utastaajabu sana kuona jinsi binadamu atakavyokuwa amepiga hatua kubwa katika ulimwengu wa sayansi.

MWISHO.

1 Comment
  1. steven m laizer says

    sasa aliens kama watatawala dunia kama nya)kati za mwisho si ni wale watu wa illuminati ndio basi watafanya hio chapa ya mnyama?

Leave A Reply