ALIKIBA HAKAMATIKI ‘YOUTUBE’, HAKAMATIKI MTAANI

ALIKIBA HAKAMATIKI

 

 

NAMBA hazidanganyi. Toka Alikiba aachie wimbo wake mpya wa Seduce Me, takribani siku mbili zilizopita, mapokezi yamekuwa makubwa na ndiye kinara wa ‘Youtube’ hivi sasa.

Siku saba zilizopita niliyatabiri haya katika makala iliyokwenda kwa jina la  MKWARA WA INSTA WA ALIKIBA UTAVUNJA UKIMYA?. Kiba kavunja ukimya wake kwa kishindo kikubwa.

MPAKA SASA VIDEO IMETAZAMWA MARA NGAPI?

Ina watazamaji wapatao milioni moja, laki nane na kumi na saba na mia tano arobaini na nne. Idadi hii inazidi kuongezeka na kusambaa zaidi kama moto wa mabua.

MTAANI HALI IKOJE?

Alikiba hakamatiki wimbo unapigwa kila kona. Mapokezi ni mazuri na watu wengi maarufu na wasio maarufu wanapongeza kazi ililyofanywa na Kiba.

ALIKIBA NDIYE MFALME?

Kutokana na ushindani mkubwa uliopo na kuwepo kwa ‘timu’ ngangari, huwa sitoi majibu ya swali hili abadani. Nawaachia wasomaji waseme wao katika nafasi ya kutoa maoni. Mara zote nilizowahi kusema nani ni mfalme nilijikuta matatani. Na katika mara zote hizo nilionewa, nikaporomoshewa matusi mazito ya nguoni!

MUZIKI WA TANZANIA UMEKUA?

Ndiyo. Hatupo tulipokuwa miaka kadhaa iliyopita. Hivi sasa tupo katika hatua ya juu kabisa. Vijana wafunge mkanda ili wazidi kuipeperusha bendera katika uwanja wa muziki, kitaifa na kimataifa.

MAKALA: DAUD MAKOBA| GPL


Loading...

Toa comment