Alikiba Kutoa PPE 200 Kupambana na Corona
STAA wa Bongo Fleva, Alikiba, amesema taasisi yake ya Kiba Foundation itatoa msaada wa mavazi 200 ya wahudumu wa afya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona (Personal Protective Equipment – PPE) ili yawasaidie wakati wa vita hii ya dunia dhidi ya virusi hivyo hasa wanapowahudumia wagonjwa wa covid-19.


