The House of Favourite Newspapers

ALIYEANZISHA KOMBE LA DUNIA HUYU HAPA

UNAPOZUNGUMZIA michuano ya soka, basi ile ya Kombe la Dunia ndiyo inashika namba moja kwa ukubwa na inapendwa sana duniani kote kwani kitendo cha timu kushiriki tu ni historia kubwa kwao.

 

Mpaka sasa ikiwa imepita takriban miaka 88, kuna nchi bado hazijashiriki michuano hiyo. Tanzania ni mojawapo. Lakini je, unamjua aliyebuni michuano hiyo? Leo unapata fursa ya kumfahamu kama ulikuwa haumfahamu.

 

Huyu anaitwa Jules Rimet ambaye ni raia wa Ufaransa. Yeye ndiye aliyekuja na ‘idea’ ya kuzikutanisha nchi kupitia mchezo wa soka kitu ambacho kilikuja kufanikiwa hadi sasa ambapo michuano hii kwa mara ya kwanza ilifanyikia nchini Uruguay mwaka 1930. Alifanya hivyo akiwa Rais wa Fifa kuanzia 1921 hadi 1954.

Comments are closed.