The House of Favourite Newspapers

Aliyefumaniwa na Hawara… Mapya Yaibuka

0

Na Dustan Shekidele, Morogoro
KATIKA hali isiyo ya kawaida, mfanyabiasha maarufu mkoani hapa, Grace Haule ‘Nyamatandala’ anamsaka mwanaume aliyedai alikuwa mumewe wa ndoa kisha kuachana, Juma Mwandaba kwa kesi inayosomeka Mor\RB\1456\2016 akimtuhumu kufanya fujo nyumbani kwake na kumpiga mpenzi wake Josse Kigenda.

Hivi karibuni gazeti ndugu na hili la Risasi Jumamosi liliripoti habari ya Mwandaba kudai kumfumania Kigenda ambaye ni mwanamuziki maarufu mkoani hapa akiwa nyumbani kwa mkewe maeneo ya Modeko ambapo mwanamke huyo alikanusha kuwa Mwandaba hana uhalali wa kuwa mumewe kwani walishaachana.

Baada ya habari hiyo kutoka, Grace anayemiliki baa kadhaa mkoani hapa na Kigenda anayetamba na wimbo wake wa ‘Mama Mkwe Kisaga Gani’ waliibuka na kumtafuta mwandishi wetu na kumpa mwendelezo wa habari hiyo.

“Wewe Shekidele (mwandishi) huyo Mwandaba si alikuita na kukupa stori na picha za utupu za Kigenda sasa njoo huku Modeko na mimi nikupe stori,” alisema Grace.
Mwandishi wetu alifika eneo hilo na kumkuta Grace.

’’Ni kweli Mwandaba ni mume wangu ambaye baada ya kunidhulumu pesa zangu alikimbia na kuibuka juzi nyumbani kwangu na kumpiga picha za utupu Kigenda ambaye nikiri kweli ni mpenzi wangu baada ya huyo Mwandaba kunikimbia miaka 3 iliyopita nikawa na huyu Kigenda,” alisema Grace na kuongeza:

“Kavamia kwangu bila taarifa na kumpiga Kigenda na baada ya kufanya tukio hilo na kukupa wewe hiyo habari akatimkia zake jijini Mwanza anakoishi, leo kafanya hivyo kesho anaweza kuja kivingine na kusababisha mauaji nyumbani kwangu, anafanya visa hivi baada ya kuniomba msamaha na mimi kumkatalia hivyo anahisi huyu Kigenda ndiye anayesababisha kushindwa kurudiana naye.”
Akihojiwa kwa njia ya simu Mwandaba alisema Grace ni mke wake wa ndoa na hajawahi kumpa talaka:

”Tumetengana kwa muda baada ya kuzuka mgogoro kwenye ndoa yetu, mimi bado ni mumewe na cheti cha ndoa ninacho, hivyo nina haki zote na mke wangu ikiwemo kufika nyumbani kwake wakati wowote na huyu Kigenda kweli nilimkuta chumbani kwa mke wangu akiwa uchi wa mnyama, niliumia sana,” alisema Mwandaba.

Leave A Reply