ALIYEGANDWA KICHWANI MAHINDI YA WIZI AACHIWA (Video)

Frank Joseph

KIJANA Frank Joseph Mkazi wa Mbezi jijini Dar aliyekuwa akishikiliwa katika Gereza la Mkuza Mkoani Pwani kwa kosa la kuiba furushi la mahindi linalokadiriwa kuwa na kilo ishirini kutoka shambazi kwa mkazi wa Mlandizi, Bi. Seva Selemani,  leo ameachiwa huru na mahakama ya Mwanzo ya Mlandizi baada ya mlalamikaji kutotokea mahakamani licha ya kuitwa kwa hati ya wito wa mahakama hiyo (summons).

 

Mtuhumiwa huyo alifunguliwa  shitaka hilo siku kadhaa zilizopita baada ya kujipeleka polisi kutokana na furushi la mahindi hayo aliyoiba kung’ang’ania kichwani na begani mwake na kushindwa kulitua.

 

Hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, Nabwike Mbaba, alisema mahakamni hapo kuwa anamuachia mshitakiwa huyo kutokana na mlalamikaji kutofika mahakamani hapo kutoa ushahidi wa jinsi alivyoibiwa.

Hali ilivyokuwa mahakamani baada ya Frank Joseph kuachiliwa huru mahakamani.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS   

Loading...


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment