The House of Favourite Newspapers

Aliyejifanya Luteni Wa Jeshi Simiyu Apandishwa Kizimbani – Video

Nchambi Nsungwa Mapanda kwa jina maarufu Emanuel Gangala (24)

Nchambi Nsungwa Mapanda kwa jina maarufu Emanuel Gangala (24) mkazi wa mtaa wa sima katika halimshauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu aliyejifanya Mwanajeshi wa JWTZ afikishwa mahakamani kwa makosa matatu.

Mwendesha mashitaka toka ofisi ya taifa mashitaka, Betrice Mboya mbele ya hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama ya mkoa wa simiyu Alex Mtenga kuwa mnamo tarehe 14.2.2025 huko katika eneo la Shule ya Sekondari Simiyu alijitambulisha kuwa yeye ni Afisa wa Jeshi la Wananchi mwenye cheo cha Luteni ambapo aliwahadaa watu mbalimbali kuwa angewasaidia kuwaingiza Jeshini na usalama wa Taifa

Huku jambo hilo likiwa ni kosa chini ya kifungu 100 [b] na kifungu 35 cha sheria ya mwenendo wa makosa jinai sura 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2022.

Aisha katika Shtaka la pili ameshtakiwa kwa kosa la kukutwa amevaa sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania.