Bashe Awapongeza Mawaziri Wateule Wizara ya Kilimo, Atoa Shukrani kwa Rais Samia

Mbunge wa Nzega na aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Hussein Mohamed Bashe ameandika ujumbe wa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa imani na kuamini kwake wakati akiwa Naibu Waziri na baadaye kuteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo.
Amesema uteuzi huo ulikuwa heshima kubwa kwake na kwamba anashukuru kwa nafasi aliyopewa ya kuwatumikia Watanzania.
Aidha, amepongeza Daniel Godfrey Chongolo kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo, akisema anamfahamu kama mkulima na mzalendo, na kuamini atasaidia Rais Samia kutimiza matarajio ya wananchi. Pia, amepongeza David Silinde kwa kuendelea kuaminiwa kama Naibu Waziri, akibainisha kuwa atakuwa msaada mkubwa kwa Waziri wake.
Mbunge huyo pia ametoa shukrani kwa watumishi wote wa Wizara ya Kilimo kwa ushirikiano wa hali ya juu waliompa katika kipindi chake cha miaka sita, na kuwaomba kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.

