Aliyemchoma Mkewe na Magunia ya Mkaa, Upelelezi Wakamilika – Video

KESI ya aliyemuua mkewe kwa kumchoma na magunia mawili ya mkaa, Said Luwongo iko mbioni kuelekea mwisho baada ya wakili wa serikali mwandamizi, Wankyo Simon kuomba kesi hiyo ipelekwe mbele ili itakaposomwa tena iwe imekamilika.

 

Kesi hiyo iliyotakiwa kusomwa leo chini ya Jaji Salum itasikilizwa tena tarehe 24/9/2019 ambapo kama alivyosema wakili, upelelezi utakuwa umekamilika kwani uko mwishoni na nyaraka muhimu zinaandaliwa ili kesi ipelekwe mahakama kuu.

 

Baada ya kuzungumza hayo, mshtakiwa aliomba nafasi ya kuzungumza jambo na baada ya kuruhusiwa alisema kuwa hapo awali aliomba kopi za kesi yake lakini hakuzipata hivyo angeomba apatiwe kopi hizo. Wakili alimjibu kwa kumwambia kuwa alimwagiza mtu ampatie kopi hizo lakini kama hakumpatia atampa yeye mwenyewe.


Loading...

Toa comment