The House of Favourite Newspapers

Aliyemtungua Manula Anapata Tabu Sana

0

OKTOBA 30, 2019, Gerald Mdamu alifunga bao lake la nne mbele ya Aishi Manula ndani ya Ligi Kuu Bara lililotibua rekodi ya Simba iliyokuwa chini ya Patrick Aussems iliyocheza mechi sita bila kufungwa.

Baada ya kumtungua bao hilo Manula mpaka leo, Mdamu hajafunga bao lingine ndani ya Ligi Kuu akibakiwa na mabao yake manne licha ya kucheza mechi nyingine, pia Januari 22 na Azam FC wakati timu yake ikifungwa bao 1-0 alikosa penalti.

Mechi ambazo Mwadui imecheza baada ya ushujaa wa mchezaji huo mpaka sasa ni 13 sawa na dakika 1,170. Mwadui imefungwa mabao 21 na kufunga mabao 11.

Imeshinda mechi moja imepoteza saba na kulazimisha sare tano ikiwa nafasi ya 19 na pointi 19, lakini bado mambo yamekuwa magumu kwa mchezaji huyo.

Matokeo yao ni kama ifuatavyo, Lipuli 2-0 Mwadui (Novemba 2), Mtibwa Sugar 1-0 Mwadui , Tanzania Prisons 1-1 Mwadui, Mbeya City 1-2 Mwadui, Mwadui 1-1 KMC, Mwadui 1-1 Ruvu Shooting .

Januari 8, Mwadui 0-1 Azam FC, Biashara United 2-1 Mwadui, Kagera Sugar 2-1 Mwadui, Singida United 2-2 Mwadui, Mwadui 0-2 Ndanda, Mwadui 1-1 Namungo na Alliance 4-1 Mwadui.

Leave A Reply