The House of Favourite Newspapers

Aliyemuingizia Mtoto Uume Mdomoni, Jela Miaka 20

0


MAHAKAMA ya Wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam imemhukumu kifungo cha miaka 20 jela mkazi wa Kimara Stop Over, Liziki Kessy,  baada ya kukutwa na hatia ya kumwingiza uume wake kwenye njia ya haja kubwa na mdomoni mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka saba ili aunyonye.

 

Hukumu hiyo imesomwa jana Jumatatu Januari 20, 2020,  na Hakimu Mkazi, Hudi Hudi,  aliyesema mahakama hiyo imemtia hatiani mshtakiwa huyo baada ya kupitia mashahidi watano wa upande wa mashtaka huku upande wa utetezi ukiwa na mashahidi watatu akiwamo mshtakiwa mwenyewe.

 

Hudi amesema amezingatia shtaka hilo na adhabu ya chini ni miaka 30 hivyo mahakama hiyo imemuhukumu mshtakiwa huyo kwenda jela miaka 20.

 

Hudi amesema baada ya kupitia upande wa ushahidi wa mashtaka na ushahidi upande wa utetezi mahakama hiyo imebaini mshtakiwa huyo alimfanyia tendo la aibu  mtoto huyo.

 

Amesema mtoto (mwathirika) aliieleza mahakama jinsi mshtakiwa alivyomwita na kumpeleka kwenye jumba bovu huku akimvua kaptura na kuanza kumwingizia uume wake kwenye njia ya haja kubwa na alipopiga kelele ndipo mshtakiwa huyo aliuingiza uume kwenye mdomo wa mtoto huyo.

 

“Ushahidi wa muathirika umeungana na ushahidi aliyoutoa mama yake mzazi pamoja na daktari wa hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala ambaye alibaini mtoto huyo alikuwa na michubuko kama kuna kitu kisicho na ncha kiliingizwa sehemu ya haja kubwa,” alisema Hudi.

 

Naye mshtakiwa  alidai yeye ni mwathirika ana ugonjwa wa kisukari na kifua kikuu (TB) na anatumia dawa hivyo asipewe adhabu kali na kwamba hana wazazi, yaani yatima.

Leave A Reply