Aliyemuua Mjukuu Wake Ahukumiwa Kunyongwa – Video

 

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemuhukumu kunyongwa hadi kufa mwanamke Esther Lyimo (47) baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mjukuu wake kwa kipigo.

Hukumu hiyo imesomwa leo Novemba 8, 2019 na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Pamela Mazengo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyopewa mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.

Baada ya kutolewa hukumu hiyo Esther ameonekana kujifunika mtandio ili wanahabari waliokuwa wakitekeleza wasiweze kumpata sura yake kwa urahisi.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on


Loading...

Toa comment