The House of Favourite Newspapers

Aliyemuua Mke Kikatili Kwenye Fumanizi Ahukumiwa Kunyongwa Hadi Kufa

0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu Dibron Said kunyongwa hadi kufa baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kumuua mkewe Herieth Justine kwa kumchoma na kisu begani, tumboni na kifuani baada ya kumfumania na mwanaume mwingine.
Hukumu hiyo imetolewa leo Januari 17, 2023 na Hakimu Mkazi Mkuu, Evodia Kyaruzi ambapo akitoa hukumu hiyo amesema kutokana na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka wa mashahidi sita pamoja na ripoti ya kitabibu ya kifo cha marehemu hivyo inamtia hatiani kwa kosa la kuua kwa kukusudia.
Hakimu Kyaruzi amesema kutokana na ushahidi uliotolewa na mjomba wa marehemu,Castoly Salum jinsi alivyoshuhudia mshtakiwa huyo akimchoma kisu mkewe hadi umauti unamkuta pamoja na ripoti ya hospitali hivyo Mahakama hiyo inamuhukumu kunyongwa hadi kufa.
Katika kesi ya msingi, Said  anadaiwa kutenda kosa lake Machi 11, 2018 katika eneo la Vingunguti ambapo anadaiwa kumuua kwa makusudi Herieth Justine, baada ya kumfumania akiwa na mwanaume mwingine.
Mshtakiwa huyo anadaiwa baada ya kutekeleza mauaji hayo, alienda kituo cha Polisi Vingunguti na kabla hajaingia ndani alijichoma kisu tumboni hadi utumbo ukatokezea kwa nje akiwa na nia ya kujiua baada ya kumfumania mke akiwa na mwanaume mwingine ndani ya nyumba yake hivyo pia Mahakama imemtia hatiani kwa makosa hayo.
Leave A Reply