The House of Favourite Newspapers

Aliyeng’atwa Ulimi Singida Akamatwa

aliyengatwaulimiSaidi Mnyambi alipofikishwa hospitali kwa mara ya kwanza.

SINGIDA, zikiwa zimepita siku saba tangu kijana Saidi Mnyambi (26) ang’atwe ulimi na jirani yake, Mwajabu Jumanne (36) hadi kupoteza uwezo wa kuongea na kula, hatimaye Jeshi la Polisi limesema linawashikilia wote wawili kwa uchunguzi zaidi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Peter Kakamba amesema polisi imelazimika kuwashikilia wote wawili kutokana na maelezo yao kutofautiana.

Alisema wakati kijana huyo anadai kuwa tukio hilo lilitokea baada ya yeye kulazimishwa kufanya mapenzi, mwanamke huyo naye anadai kuwa alimng’ata ulimi wakati akijaribu kujiokoa ili asibakwe.

Kutokana na hali hiyo, Kamanda Kakamba alisema jeshi hilo limeona kuna haja ya kuwashikilia wote wawili kwa uchunguzi zaidi ili kubaini ukweli wa jambo hilo kabla ya kuwafikisha mbele ya Mahakama.

Mnyambi alinyofolewa theluthi moja ya ulimi wake na mke wa jirani yake kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kumlazimisha kufanya naye mapenzi Sikukuu ya Idd El Hajj saa 3.30 usiku.

Alidai kuwa siku ya tukio, mwanamke huyo alimwomba amsindikize nyumbani kwake kwa kuwa alikuwa amelewa.

Hata hivyo, walipofika njiani inadaiwa kuwa mama huyo alimtaka kijana huyo wafanye mapenzi jambo ambalo alimkatalia lakini akamwomba waagane, angalau kwa kunyonyana ulimi (ampe denda), lakini ghafla kijana huyo alishtukia aking’atwa ulimi na mama huyo na kukimbilia nyumbani kwake.

Muuguzi Mwandamizi Hospitali ya Mkoa wa Singida alikolazwa kijana huyo, Herman Mallya amesema kuwa hali ya mgonjwa huyo inaendelea vizuri ingawa hajapata uwezo wa kuongea.

 

Comments are closed.