Aliyepokea Fedha Kimakosa kwa M-Pesa Ashtakiwa

STANLEY IRUNGU amefikishwa mahakamani jijini Nairibo, nchini Kenya, baada ya kuchukua Sh. 39,000 za Kenya (Shilingi za Tanzania 1,300,000/=) katika Sh. 60,000 za Kenya,  kwa M-pesa kutoka kwa mwanamke mmoja ambaye ni mfanyabiashara aliyezituma kimakosa kwake.

 

Millicent Atieno ambaye ni mfanyabiashara alikosea kutuma fedha hizo lakini aliwasiliana na Kampuni ya Mawasiliano ya Safaricom ambao walimrudishia kiasi cha Sh. 21,000 za Kenya (Shilingi za Tanzania 465,000/=) kilichobaki.

 

Katika kumtafuta Irungu ili arudishe fedha hizo, kampuni hiyo ilimpigia simu mara kadhaa lakini hakuzipokea.  Hata hivyo, baadaye alipatikana na akakiri kuchukua kiasi hicho na kuahidi kwamba atakirudisha.

Mahakama ilimwachia kwa dhamana baada ya kutimiza masharti na kesi itatajwa Oktoba Mosi, mwaka huu.

 

 


Loading...

Toa comment