The House of Favourite Newspapers

Aliyerekodi Video Ya George Floyd Akiuawa Aula

0

Kwenye maisha usikate tamaa kwani tukio moja tu, laweza kubadilisha kabisa taswira yako. Ndicho kinachotokea kwa Darnella Frazier ambaye ndiye  alipiga picha wakati Mmarekani mweusi, George Floyd akiuawa na Polisi.

Unaambiwa Darnella ameula baada ya kushinda tuzo maalum kutoka kwenye Tuzo za Pulitzer zilizotolewa usiku wa kuamkia leo.

Tuzo za Pulitzer ndiZo tuzo za kifahari zaidi katika uandishi wa habari nchini Marekani.

Bodi inayoratibu tuzo hizo ilisema Darnella ambaye siyo Mwandishi wa Habari, lakini aliheshimiwa kwa ujasiri wa kurekodi mauaji ya George Floyd, video ambayo ilichochea maandamano dhidi ya ukatili wa Polisi ulimwenguni, ikionesha jukumu muhimu la raia katika harakati za waandishi wa habari za ukweli na haki.

Kutokana na tuzo hiyo, sasa Darnella amekuwa maarufu duniani, lakini kabla ya hapo hakuna aliyemfahamu.

STORI NA SIFAEL PAUL | GPL

MTOTO wa UWOYA AONGEA KIINGEREZA kwa KUJIAMINI, Ataja ANACHOPENDA kwa MAMA YAKE..

Leave A Reply