The House of Favourite Newspapers

Aliyesakwa Miaka 12 na FBI kwa Mauaji ya Watoto Wake Anaswa!

0

DEREVA wa teksi, Yaser Abdel Said (63),  aliyekuwa akisakwa na Shirika la Upelelezi la Marekani  (FBI) kwa tuhuma za mauaji ya mabinti zake wawili miaka 12 iliyopita kwa kuwapiga risasi amekamatwa baada ya kukimbilia mafichoni.

 

Waranti ya kumkamata Yaser Abdel mwaka 2008 baada ya kuwapiga risasi binti zake, Sarah Yaser Said, 17, na Amina Yaser Said, 18. Mshukiwa huyo ambaye ni mzaliwa wa Misri aliwekwa kwenye orodha ya FBI, ya watu 10 wanaotafutwa zaidi mwaka 2014. Yaser hivi karibuni atahamishwa Kaunti ya Dallas, ilisema taarifa iliyotolewa na Idara ya FBI Dallas.

Jopo kazi la uhalifu  linaloongozwa na FBI mjini Dallas limekuwa likimtafuta kwa muda mrefu Yaser Abdel,” alisema ajenti maalum wa FBI Dallas, Matthew DeSarno.

 

Mama ya wasichana hao, Patricia Owens, amesema amefurahishwa na hatua ya kukamatwa kwake, na kuviambia vyombo vya habari vya mji huo: “Sasa wasichana wanaweza kupumuzika kwa amani.”

 

Islam Said, mtoto wa kiume wa mshukiwa, na Yassim Said pamoja na ndugu mmoja wa mshukiwa walishitakiwa kwa kumficha jamaa huyo. Uchunguzi wa mauaji ulianzishwa Januari 1, 2008 baada ya Amina na Sarah kupatikana wakiwa wameuawa kwa kupigwa risasi.

 

Siku hiyo, mshukiwa aliwabeba kwenye teksi wasichana hao kwa kisingizio kwamba anaenda kuwanunulia chakula. FBI inasema aliwapeleka hadi Irving, Texas, ambako inadaiwa aliwapiga risasi wasichana hao ndani ya gari. Wote walifariki kutokana na majeraha kadhaa ya risasi.

Kabla ya vifo vyao, jamaa wa familia aliwaambia polisi kwamba mshukiwa alitishia “kumdhuru” Sarah kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtu ambaye si Muislamu, kwa mujibu wa kituo cha habari cha CBC. Mauaji ya mwanafamilia anayedhaniwa kufedhehesha jamaa zake wakati mwingine husemekana kuwa “mauaji ya heshima” – lakini wakosoaji wanapinga maana inayotolewa kwa mauaji kama hayo.

 

Idara ya polisi ya Irving ilifanya uchunguzi wa mauaji ya Amina na Sarah na, kufikia Januari 2, 2008 waranti ya kukamatwa kwa Yaser Abdel Said ilitolewa. Tangu wakati huo, mawakala wa FBI “wamekuwa wakipambana kuwatafutia haki Amina na Sarah”, Mkuu wa Idara ya polisi ya Irving Jeff Spivey, alisema.

Leave A Reply