The House of Favourite Newspapers

Aliyetobolewa Macho na ‘Scorpioni’ Aanza Kutoa Ushahidi Mahakamani

scorpioni-6NA DENIS MTIMA | GPL;

Dar es Salaam: KESI ambayo imekuwa ikivuta hisia za watu wengi jijini Dar na maeneo mengine kuhusu Salum Njwete ‘Scorpion’ ambaye anakabiliwa na kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kudaiwa kumjeruhi, Said Mrisho,  ambaye kwa sasa amepata ulemavu wa macho baada ya kutobolewa macho.

salum-mrisho  Kijana Said Mrisho anayedaiwa kujeruhiwa na kutobolewa macho na Salumu maarufu kama Scorpion (katikati), akisaidiwa na ndugu zake (Picha na Maktaba)

Kwa mara ya kwanza, shahidi namba moja upande mshtaki wa kesi hiyo ambaye ni Said Mrisho (aliyetobolewa macho) ametoa ushahidi wake mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ya Wilaya ya Ilala na kuiambia mahakama kisa chote kilichotokea hadi kutobolewa macho.

scorpioni-2

Mshtakiwa Salum Njwete ‘Sorpion’ akifikishwa mahakamani.

Katika kesi hiyo, inadaiwa kuwa zaidi ya mashahidi sita wanatarajiwa  kutoa ushahidi wao wa kumtetea Said Mrisho aliyetobolewa macho.

scorpioni-3Baada ya kusikiliza hoja za shahidi huyo, Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ya Wilaya ya Ilala anayesikiliza kesi hiyo, Flora Haule, ameahidi kuwa ataendelea kusikiliza mashahidi wengine wa kesi hiyo, ambapo baadaye aliahirisha kesi hiyo na itatajwa tena Desemba 27 mwaka huu.

scorpioni-7Kwa upande mwingine, mshtakiwa wa kesi hiyo, Salum Njwete ‘Scorpion’ aliyefikishwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la Magereza, hakutakiwa kujibu chochote zaidi ya kusikiliza na kurudishwa lupango.

scorpioni-9Scorpion anazidi kusota lupango toka kesi hiyo ianze huku ikivuta hisia za watu wengi ambao wamekuwa wakijitokeza mahakamani kuisikiliza wakiwemo ndugu zake na wale wa upande wa Said ambapo imekuwa.

scorpioni-1Baadhi ya ndugu na wanahabari waliofika mahakamani hapo kusikilza kesi hiyo.

halotel-strip-1-1

Darassa Afunguka Tuhuma za Kuiba Beat ya Saida Karoli Kwenye Wimbo Wake wa Muziki

Comments are closed.