The House of Favourite Newspapers

Aliyeua Watu 59, Kujeruhi 527 Las Vegas Alikuwa Bilionea

0

MTU ambaye Jumapili iliyopita usiku aliua watu 59 na kujeruhi 527 kwa bunduki jijini Las Vegas, Marekani, alikuwa ni tajiri mkubwa ambaye alikuwa amejaza bunduki 23 kwenye chumba chake cha hoteli ya Mandalay Bay ambacho alikigeuza kuwa kiota cha  kudungulia ambapo alifyatua risasi kwenye umati wa watu waliokuwa kwenye tamasha la muziki.

 

Muuaji huyo, Stephen Paddock, 64, alikutwa na polisi amejiua wakati wanaingia katika chumba chake kilichokuwa ghorofa ya 32 cha Hoteli ya Mandalay Bay.

Kwa nini Paddock aliamua kufanya mauaji hayo, bado haieleweki, kwani, kwa mujibu wa kaka yake, hakuwa na mahusiano yoyote ya kidini au kisiasa, hakuwahi kupitia jeshini isipokuwa alikuwa na bastola kadhaa tu.

 

Japokuwa wapiganaji wenye kutaka kuanzisha  dola ya Kiislam (ISIS) wamedai kuhusika na mauaji hayo, wakisema Paddock alikuwa amebadili dini na kuwa Mwislam, kaka yake na mamlaka ya serikali sehemu aliyokuwa anaishi wamekanusha jambo hilo.

 

Jamaa huyo, Stephen Paddock, 64, alipata utajiri mkubwa kutokana na kumiliki majumba na mashamba, na kwa mujibu wa kaka yake, alikuwa pia anamiliki ndege mbili na mali kadhaa nchini Marekani ambapo alikuwa anaishi maisha ya  kawaida licha ya kuwa alikuwa anapenda kucheza kamari.

Pia anasemekana alikuwa amelimbikiza kwa siri bunduki 42, miongoni mwake zikiwemo bunduki za kufyatua risasi mfululizo na zenye darubini maalum.

Alizipeleka kwa siri bunduki 23 kwenye chumba chake cha hoteli ya Mandalay Bay na kuweka bunduki mbili aina ya ‘rifle’ kwenye kiweko maalum cha miguu mitatu sehemu ya dirishani kuelekea sehemu lilipofanyika tamasha la muziki lililokuwa linajulikana kama Route 91 Harvest.

Maelfu ya risasi pia yalikutwa kwenye chumba hicho kwa ajili ya kutekelezxa mauaji hayo. Vilevile, gari lake lilikutwa likiwa na aina ya mbolea ambayo hutumika kutengenezea mabomu.

 

Paddock alikuwa ameishi sehemu 27 kwenye majimbo ya Nevada, Florida na Texas na alikuwa ameishi maisha ya kimya na yasiyokuwa na umaarufu, hivyo sababu ya yeye kufanya mauaji hayo ni kitendawili.

 

Leave A Reply