The House of Favourite Newspapers

Aliyewahi Kugombea Uspika Atunukiwa Tuzo ya Uhodari na Shirika la Viwango (TBS)

0

 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Mhandisi Johanes Maganga (kushoto), akikabidhi Tuzo ya Mfanyakazi Hodari kwa Hamis Sadiki

 

 

 

 

 

Hamisi Sadiki ambaye alikuwa miongoni mwa waliowania nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM miezi kadhaa iliyopita, amechaguliwa kuwa mfanyakazi hodari wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na kupewa tuzo.

Hamis amepewa tuzo hiyo katika sherehe za utoaji wa Tuzo za Mfanyakazi Hodari wa TBS kwa mwaka 2021/2022 zilizofanyika mkoani Morogoro jana Juni 21, 2022.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Mhandisi Johanes Maganga amesema Hamis ni afisa utumishi ambaye amekuwa akijitoa na kuonesha kipaji kikubwa katika kusimamia rasilimali watu kwa kuhakikisha anafuatilia na kutatua changamoto mbalimbali za kiutumishi.

“Hamisi ni mbobezi, mtaalam mahiri na hazina ya taifa na ninamuona akifika mbali sana siku za usoni, ni kongozi mpole, mnyenyekevu, msikivu na mwenye kutumia taaluma yake vyema kwa maendeleo ya taifa letu,” amesema Maganga.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo, Hamisi amesema menejimenti ya TBS imekuwa ikimpa sapoti kubwa katika kutekeleza majukumu yake na kuahidi kuongeza kasi zaidi katika kutatua changamoto za wafanyakazi ndani na nje ya shirika ili kuhakikisha utumishi wa umma unazidi kuwa kimbilio la Watanzania wote katika kupata huduma zilizotukuka.

Leave A Reply