The House of Favourite Newspapers

Ali Kamwe Akamatwa Na Polisi Tabora, Atupwa Selo, Kauli Yake Iliyomponza Ni Hii Hapa – Video


Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga SC, Ally Kamwe, amekamatwa na vyombo vya usalama kwa tuhuma za kutoa lugha chafu kwa viongozi wa kiserikali.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa Kamwe alikamatwa jana April 2, 2025 baada ya kumalizika kwa mechi kati ya Yanga na Tabora United na kupelekwa katika kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi.

Kwa mujibu wa vyanzo vya karibu na klabu, tukio hilo limeibua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki wa soka nchini, hasa wafuasi wa Yanga SC, ambao wanataka ufafanuzi juu ya hali halisi ya tukio hilo.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora, limethibitisha kukamatwa kwa Kamwe kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Mpaka sasa, uongozi wa Yanga SC haujatoa tamko rasmi kuhusu suala hilo, huku mashabiki wakingoja kwa hamu kujua hatma ya Kamwe na iwapo ataachiwa au kufikishwa mahakamani.

Endelea kuwa nasi kwa taarifa zaidi kuhusu tukio hilo.