The House of Favourite Newspapers

ALP Yazindua Ripoti Ya Soko La Pamoja La Afrika ya Mashariki

0
Watendaji mbalimbali wakionyesha shahada ya kuzinduliwa kwa soko la pamoja la Afrika ya Mashariki – Huduma na Bidhaa za Afrika yaMashariki, kutoka kushoto ni Francis Gimara, Mtendaji Mkuu ALP Afrika Mashariki, Herry Onoria, Mkuu wa Maudhui na Ujuzi ALP Afrika Mashariki, Christine Mutimura, Msajili EACJ, Solagbade Sogbetun, Mmoja wa wamilikiwa ALP Nigeria, Herman Kasekende, Mkurugenzi Mtendaji benki ya Standard Charted na Claude Ndahangarwa, Mkurugenzi wa Leaf, Tobacco and Commodities.

Dar es Salaam, Mei 18, 2023. Kampuni inayojihusisha na usimamizi wa shughuli za kisheria katika nchi za Afrika ya Mashariki, ALP East Africa, imezindua ripoti inayohusu taarifa za soko la Pamoja la Afrika ya Mashariki kuangazia huduma na bidhaa katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa ripoti hiyo Mkuu wa kampuni ya ALP East Africa, Bw. Francis Gimara amebainisha kuwa, “Dhumuni la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ni maingiliano ya ushirikiano wa kiuchumi na maingiliano ya ushirikiano wa kibiashara, ikiwa ni dhumuni la msingi, kama sio la kwanza, la lengo la mchakato wa maingiliano.

Wadau katika picha ya pamoja.

Maingiliano ya kibiashara ndio msingi wa Mkataba na itifaki za Umoja wa Soko la Pamoja na Forodha, na unatarajiwa kuwa mhimili mkuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.”

“Tukiwakama watoa huduma zenye maingiliano na ushauri wa kitaalamu wa makampuni ya kisheria kwenye nchi za Uganda, Kenya, Tanzania na Sudani ya Kusini — ALP ni kampuni inayotoa huduma za kisheria na ushauri kwenye nchi hizi kwa upande wa biashara pamoja na kuanzisha biashara mpya na usimamizi wake.

Jukwaa la majadiliano.

Msaada wa kiushauri kuhusiana na biashara pamoja shughuli za kibiashara baina ya nchi moja na nyingine ni eneo ambalo ALP East Africa ambalo inalishughulikia mara kwa mara hususani kupitia sheria na tarataibu za kiudhibiti za nchi wanachama wa Afrika ya Mashariki,” aliendelea Bw. Gimara.

ALP East Africa inazingatia upitiaji wa Huduma za Soko la Pamoja la Afrika ya Mashariki na kutoa uelewa wa uhusiano kati ya mifumo ya udhibiti wa kitaifa na mfumo wa biashara wa kikanda (Jumuiya ya Afrika Mashariki).

“ALP East Africa inaelewa umuhimu wa wadau katika maeneo ya biashara—katika maoni ya umma, serikali za Jumuiya ya Afrika Mashariki (ikiwa ni pamoja na watendaji wao mbalimbali na wa ngazi tofauti) na, kwa mtazamo binafsi, watendaji wa sekta binafsi (wawekezaji, jumuiya ya wafanyabiashara, na kadhalika,” alimalizia Mkuu huyo.

Kampuni hiyo imetoa ripoti ya Soko la Pamoja la Huduma na Bidhaa za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC CSG Scan) 2022 – 2023 kama sehemu ya usaidizi wake wa ushauri wa kisheria wa mara kwa mara wa kuhusu ushirikiano wa biashara wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.

Kama hatua ya kwanza, Soko la Pamoja la Bidhaa na Huduma la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC CSG Scan) 2022 – 2023 linatathmini hatua za udhibiti kulingana na sheria, notisi za kiutawala, maagizo, n.k — zilizochukuliwa na nchi tano Wanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ambazo zinaathiri usafirishaji huru wa mtaji, bidhaa na huduma katika soko la pamoja katika kipindi cha Januari mpaka Desemba 2022.

Nchi wanachama zilizozingatiwa katika uzinduzi na uchunguzi wa awali wa Huduma na Bidhaa za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki wa kila mwaka ni Kenya, Rwanda, Tanzania, Sudan Kusini, na Uganda. Mipango iliyopo ni ALP East Africa inapanga kutoaripotiyanamnahii kila robo ya mwaka.

Ripoti ya Soko la Pamoja la Huduma na Bidhaa la Jumuiya ya Mashariki (EAC CSG Scan) 2022 – 2023 imezinduliwa kama utangulizi mpana wa ALP East Africa katika nchi kadhaa wanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki na kuzitaka kujikita katika huduma na bidhaa za pamoja chini ya soko la pamoja manufaa yake makubwa kwa hatua za maingiliano ya kibiashara ya sekretarieti za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, Baraza la Sheria la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, Baraza la Mawaziri na taasisi nyingine za kijumuiya.

Uzinduzi wa soko la pamoja la huduma na bidhaa za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki 2022 – 2023 ulihudhuriwa na maafisa wa sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, wajumbe wa Baraza la Sheria la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, asasi za kiraia, sekta za biashara n.k.

Leave A Reply