Amanda apungua kilo 11 mwilini

amandaMwandishi wetu

MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’ amejikondesha makusudi na kufanikiwa kupunguza kilo 11 mwilini.

Akizungumza na mwanahabari wetu, Amanda alisema baada ya kuona mwili unazidi kunenepa na ‘ubonge nyanya’ unamnyima uhuru, aliamua kutafuta ‘gym’ mitaa ya nyumbani kwake, Mbezi Beach jijini Dar ambayo ilimsaidia kufanya mazoezi pamoja na vyakula maalum ambavyo vilichangia kwa kiasi kikubwa kupunguza uzito huo.

“Ubonge niliona unanitesa, nikaamua kufanya mazoezi kwa miezi michache tu na kula vyakula nilivyopangiwa. Namshukuru Mungu nimepungua kilo 11 na bado nataka nipungue zaidi,” alisema Amanda.

Awali,  mwigizaji huyo alikuwa na uzito wa kilo 89 lakini sasa amepungua hadi kufikia kilo 78.

Loading...

Toa comment