Debora Mhagama (kushoto) akisaidiwa kujaza kuponi na Ofisa Masoko wa Global, Yohana Mkanda.
Joshua Benjamin (kushoto) akijaza kuponi kushiriki bahati nasibu ya Shinda Nyumba.
Mkanda (kulia) akimwonesha msomaji wa Amani, Issa Hamad, sehemu yenye kuponi ya bahati nasibu.
Hamadi akijaza kuponi yake.
Mkanda (kulia) akimfafanulia jambo msomaji wa gazeti la Amani namna ya kushiriki bahati nasibu hiyo.
John Helbert mkazi wa Kunduchi Dar akijaza kuponi.
Msomaji wa gazeti la Amani mkazi wa Kunduchi Dar ambaye jina lake halikujulikana (kulia) akijaza kuponi.
Mkanda (kushoto) akimsaidia msomaji kukata kuponi baada ya kumaliza kuijaza.
Hamisi Shabani (kulia) akishiriki kujaza kuponi ili kushiriki bahati nasibu ya Shinda Nyumba.
NI hatua za mwisho za lala-salama ambapo zimebaki siku 12 kuchezeshwa droo kubwa ya bahati nasibu ya ‘Shinda Nyumba’ na jana Alhamisi promosheni ya shindano hilo inayoendelea iliwafikia wakazi wa Kunduchi, Dar, waliojitokeza kwenye gari la matangazo kuchangamkia gazeti la Amani na kushiriki kujaza kuponi za bahati nasibu.
Bahati nasibu hiyo inaendeshwa na Kampuni ya Global Publishers wachapishaji wa magazeti ya Championi, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Ijumaa Wikienda.
Maofisa masoko wa Global Publishers,Yohana Mkanda na Jimmy Haroub waliwafikia wasomaji katika mitaa mbalimbali ya maeneo ya Kunduchi na kuwahamasisha kushiriki bahati nasibu hiyo.
Katika uhamasishaji huo, Yohana Mkanda alirudia wito wake kwamba: “Siku zimebaki 12 nunueni magazeti ya Global mengi na mjaze kuponi ili kujiongezea nafasi ya kushinda nyumba kwani unaweza kuwa wewe au yule na kugeuka baba au mama mwenye nyumba! Kazi kwako, nyumba ndiyo hiyoo…!!!”
Naye Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho, juzi Jumatano akizungumza na wanahabari baada ya kutembelea nyumba hiyo eneo ilipo kwa ajili ya kuona mandhari na samani zilizomo ndani ya nyumba hiyo iliyoko Salasala alisema:
“Nyumba hiyo iko tayari kukabidhiwa mshindi atakayepatikana katika droo inayotarajiwa kufanyika Juni 30 mwaka huu kwenye viwanja vya Mbagala- Zakhem jijini Dar,”
NA DENIS MTIMA/GPL

