Kama kawaida leo Alamisi, novemba 8, 2018 kikosi kazi cha promosheni ya magazeti ya Global Publishers wachapishaji wa magazeti ya Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Amani, Risasi, Uwazi, Championi na Spotu Xtra kiliingia tena mitaani na kulinadi gazeti la Amani na Spoti Xtra.
Promosheni ilifanyika sehemu mbalimbali za jiji la Dar, ikiwemo Tandale, Manzese, Magomeni, Tabata na sehemu nyingine ambapo magazeti hayo yalionekana kuwa gumzo kila kona ambako yaipita.
Katika promosheni hiyo wasomaji walionekana kugombea magazeti hayo ambapo kama kawaida waliyamwagia sifa kemkem kutoakana na habari zake za ukweli na uhakika.
Kwa upande wa Gazeti la amani limesheheni habari za kitaifa na kimataifa, matukio ya kijamii, stori, makala za burudani, mastaa wa Bongo na nje ya Tanzania, hadithi za kusisimua, katuni na vichekesho.
Nalo Gazeti la Spoti Xtra limesheheni habari ‘current’ za michezo, tetesi za usajili wa wachezaji wa Ulaya na Ligi Kuu ya Tanzania, Misimamo ya ligi, Matokeo ya mechi zote kali duniani, takwimu za michezo na uchambuzi unaofanywa na wahariri waliyobobea katika tasnia ya habari za michezo.
Wasomaji hao waliwaomba maofisa waliokuwa katika kikosi hicho kuongeza wauzaji wa magazeti hayi ili yaweze kuwafikia kiurahisi kila kona.
Spoti Xtra linakuwa mtaani kila Alhamisi ya wiki kwa bei ya Tsh. 500 na Gazeti la Amani kwa Tsh. 800/=.
HABARI/PICHA : RICHARD BUKOS / GPL
Comments are closed.