AMANI, SPOTI XTRA SASA NI GUMZO KILA KONA

Mpishi wa chapati zenye ubora wa aina yake katika maeneo ya Tandale Uzuri jijini Dar, Asia Mohammed, akifurahia jambo wakati akisoma Gazeti la Amani.

Kama kawaida leo Alamisi, novemba 8, 2018 kikosi kazi cha promosheni ya magazeti ya Global Publishers wachapishaji wa magazeti ya Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Amani, Risasi, Uwazi, Championi na Spotu Xtra kiliingia tena mitaani na kulinadi gazeti la Amani na Spoti Xtra.

Wasomaji wa Tandale Uwanja wa Fisi, waki-enjoy kusoma Gazeti la Spoti Xtra.

Promosheni ilifanyika sehemu mbalimbali za jiji la Dar, ikiwemo Tandale, Manzese, Magomeni, Tabata na sehemu nyingine ambapo magazeti hayo yalionekana kuwa gumzo kila kona ambako yaipita.

Wasomaji wa Soko la Tandale, wakifuatilia Gazeti la Spoti Xtra.

 

Katika promosheni hiyo wasomaji walionekana kugombea magazeti hayo ambapo kama kawaida waliyamwagia sifa kemkem kutoakana na habari zake za ukweli na uhakika.

Wasomaji wa Tandale Mbokomu wakifuatilia mambo yaliyomo ndani ya Spoti Xtra.

Kwa upande wa Gazeti la amani limesheheni habari za kitaifa na kimataifa, matukio ya kijamii, stori, makala za burudani, mastaa wa Bongo na nje ya Tanzania, hadithi za kusisimua, katuni na vichekesho.

Wakaka wa Tandale Uwanja wa Fisi, wakisoma Spoti Xtra.

Nalo Gazeti la Spoti Xtra limesheheni habari ‘current’ za michezo, tetesi za usajili wa wachezaji wa Ulaya na Ligi Kuu ya Tanzania, Misimamo ya ligi, Matokeo ya mechi zote kali duniani, takwimu za michezo na uchambuzi unaofanywa na wahariri waliyobobea katika tasnia ya habari za michezo.

Ofisa Mauzo wa Global Publishers, Songoro Bilal (katikati) akiwaelekeza jambo wasomaji wa Sinza White Inn.

Wasomaji hao waliwaomba maofisa waliokuwa katika kikosi hicho kuongeza wauzaji wa magazeti hayi ili yaweze kuwafikia kiurahisi kila kona.

Wasomaji wa Tandale Uzuri wakisoma Spoti Xtra.

Spoti Xtra linakuwa mtaani kila Alhamisi ya wiki kwa bei ya Tsh. 500 na Gazeti la Amani kwa Tsh. 800/=.

Mfabiashara wa Tandale Uwanja wa Fisi akifuatilia yaliyomo kwenye Gazeti la Spoti Xtra.

 

Vijana wa Manzese Bakhresa wakifuatilia yaliyomo kwenye Gazeti la Spoti Xtra.

HABARI/PICHA : RICHARD BUKOS / GPL

Toa comment