The House of Favourite Newspapers

AMANI, SPOTI XTRA YAZIDI KUKIMBIZA KITAANI

Wasomaji wa Yombo Kwa Chande jijini Dar es Salaam  wakifuatilia magazeti ya Global, Amani na Spoti Xtra.

Kikosi cha mauzo cha Kampuni ya Magazeti nya Global Publishers Ltd (GPL) watoaji wa magazeti ya Amani, Uwazi, Risasi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Championi na Spoti Xtra leo Alhamisi kiliingia tena mtaani katika sehemu  mbalimbali za Jiji la Dar es Salaam ambapo  gazeti la Amani na Spoti Xtra hutoka siku ya Alhamisi na ambapo kila kona wasomaji walionekana kuyachangamkia.

 

Wasomaji wa Yombo Reli,wakijisomea Spoti Xtra.

Baadhi ya maeneo yaliyofikiwa na kikosi cha mauzo cha GPL  ni pamoja Tabata Baracuda, Vingunguti, Kiwalani, Yombo Vituka, Buza na maeneo mengine ambapo wasomaji walionaswa maeneo hayo walitoa pongezi zao kwa waandaaji wa magazeti hayo yaliyosheheni habari za burudani, katuni, hadithi za kusisimua na mengineyo.

Kikosi cha mauzo kiliendelea kuwakumbusha wasomaji wa gazeti la Spoti Xtra kutosahau kujaza kuponi iliyopo ukurasa wa pili ambayo itawawezesha kushinda jezi za timu kubwa duniani.

Matukio katika Picha:

Wachezaji wa timu ya Beach Kauzu FC ya Yombo-Vituka wakiwa makini na Spoti Xtra baada ya kutembelewa na kikosi cha mauzo.

Wasomaji wa Vingunguti Darajani wakisoma magazeti ya Global.
Msomaji wa Vingunguti Darajani akisoma Spoti Xtra; kulia ni Ofisa Mauzo wa Global, Songoro Bilal.

Ofisa mauzo wa Global, Mussa Mgema (katikati) akiwaelekeza wasomaji jinsi ya kujaza kuponi iliyopo kwenye gazeti la Spoti Xtra ili waweze kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo jezi za timu maarufu ulimwenguni na zawadi nyinginezo.

…Akiwauzia magazeti wasomaji wa Vingunguti Darajani.

Mama Yusra wa duka la Nyamigogo lililopo Yombo-Kijiwe Samri akipata uhondo wa gazeti la Amani.   

PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS

     

 

 

Comments are closed.