The House of Favourite Newspapers

Amber aangukia kwa mume wa dada wa Kim

0

amber Mrembo Amber Rose.

LAS VEGAS, Marekani.
WANAZUNGUKANA! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia mrembo Amber Rose, kuripotiwa kuwa alijiachia na Scott Disick ambaye ni mume wa zamani wa dada yake na Kim Kardashian, Kourtney Kardashian.

rs_464x749-141029104030-rs_634x1024-140603134516-634.2kourtney-kardashian-khloe-hamptons.ls.6314 Scott Disick.

Tayari duara linazidi kuchorwa kwenye uhusiano huo kwani Kim sasa ameolewa na aliyekuwa mpenzi wa Amber, Kanye West hivyo inaonekana sasa ni mwendo wa kulipana visasi baina ya familia ya Kardashian na jeshi la mtu mmoja, Amber.
Chanzo cha karibu na mrembo huyo kilidai kuwa, wawili hao walionekana wakiwa pamoja huko Las Vegas Alhamisi iliyopita wakijiachia kama wapenzi.
Hata hivyo, Amber ambaye ni mama wa mtoto mmoja aliyezaa na Wiz Khalifa, alikana kujiachia na Scott lakini alimsifia kuwa ni kijana mzuri na aliwahi kukutana naye mara tatu tu na ni rafiki tu wa kawaida.

Leave A Reply