The House of Favourite Newspapers

Amber Lulu Afanya Uchafu

amber-lulu-2

 Na Imelda Mtema, | Gazeti la Risasi Mchanganyiko

DAR ES SALAAM: Video Queen mwenye vituko kila kukicha, Lulu Euggen ‘Amber Lulu’ Jumapili iliyopita alibambwa usiku wa manane  akifanya vitendo vichafu na msanii wa tamthiya ya Kelele aliyejulikana kwa jina moja la Talik, nje ya ukumbi wa Catalunya uliopo Mwenge Jijini Dar.

amber-lulu-5Wawili hao wakijibebisha nyuma ya gari.

Video Queen huyo alikuwa ni mmoja wa waalikwa kwenye sherehe ya kuzaliwa staa wa Bongo Muvi Irene  Uwoya, ambapo baada ya kuingia na kupata ulabu kiasi cha kutosha, alitoka nje na kukaa pembeni ya gari akiwa na msanii huyo huku wakipigana mabusu mdomoni bila kujali wapita njia.

amber-lulu-6“Nyie huyu Lulu atakuwa amepagawa kabisa maana hata haogopi kabisa kama watu wanapita na kuwaona wanachofanya, na wakati huyu sasa hivi anajinadi yuko na Young D” alisikika kijana mmoja akizungumza.

amber-lulu-1Licha ya binti huyo kuhusishwa na Young D, zipo tetesi pia zinazomtaja msanii wa Hip Hop, Roma Mkatoliki kuwa pia anatoka naye kimahaba.

amber-lulu-7Mwandishi wa habari hii alimsogelea Lulu na kutaka kujua kulikoni kufanya mambo hayo hadharani, ambapo aligeuka mbogo na kutaka aachwe aendelee na mambo yake.

amber-lulu-8“Dada yangu nakuheshimu, naomba uniache, tena uniache kabisa, hakuna aliyenilipia nauli ya kuja hapa hata mara moja,” alisema Lulu.

amber-lulu-4Katika pati hiyo iliyohudhuriwa na mastaa kibao, waalikwa walikunywa na kula kwa muda wote kuanzia saa nne usiku hadi jua linachomoza, asubuhi ya Jumatatu. amber-lulu-3Wakijiachia kima-lovee.

Comments are closed.