Amber Lulu Afunguka Kubeba Mimba ya Uchebe!

Pisi kali kunako Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Amber Lulu’ amefunguka juu ya tetesi zinazosa-mbaa kuwa amebeba ujauzito wa aliyekuwa mume wa staa mwenzake, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, Ashraf Uchebe.

 

Awali zilianza tetesi kuwa, Amber Lulu na Uchebe wapo kwenye uhusiano wa kimapenzi huku mrembo huyo akimsifia jamaa huyo kwamba ana kifua cha chuma.

 

Katika mahojiano maalum na Gazeti la IJUMAA, Amber Lulu ambaye hakaukiwi vitimbi amesema hana uhakika kama aliwahi kuwa kwenye mapenzi na Uchebe, labda kama alikuwa amelewa.

“Mimi sina mimba, kwa nini nifiche? Mimi sina mimba, sina vitu hivyo mimi,” amesema Amber Lulu.

 

Kwa muda mrefu Amber Lulu amekuwa akilia kuwa anatamani kuwa na mtoto huku akiweka wazi hisia zake kwamba, anatamani siku moja azae na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Stori:IMELDA MTEMA, Ijuma

PART 2: MBOSSO Afichua SIRI Nzito ya BOSS MARTHA – “NAJUTA, Nikikaa NALIA sana, NDUGU Wamenikana”

Toa comment