AMBER LULU AJUTA KUPOTEZA MUDA KWA PREZZO

Lulu Auggen ‘Amber Lulu’

 MAJUTO! Msanii wa Bongo Fleva, Lulu Auggen ‘Amber Lulu’ amefunguka kuwa anajuta kupoteza muda wake kwa aliyekuwa mpenzi wake, Jackson Makini ‘Prezzo’ ambaye ni mwanamuziki kutoka Kenya.

 

Akistorisha na Gazeti la Ijumaa, Amber Lulu aliyedumu na Prezzo kwa miezi kadhaa kabla ya kumwagana alisema kuwa, wakati akiwa na jamaa huyo alijishusha mno akiamini watadumu, lakini sasa ameamua kumwaga manyanga moja kwa moja na hataki tena kumsikia.

 

“Kama ni kuumia, nimeumia sana kwa yule kaka (Prezzo), mwisho wa siku nimegundua nimepoteza muda wangu mwingi sana, kumbe mapenzi hayakuwepo hata chembe,” alisema Amber Lulu anayekimbiza na Ngoma za Jini Kisirani na Mtakoma.


Loading...

Toa comment