Amber Lulu Ana Msitu Kwapani

 

HAYA ni makubwa! Msikie msanii anayefanya poa kunako Bongo Fleva, Lulu Auggen ‘Amber lulu’ amesema ameshindwa kujifanyia usafi kiasi cha kuwa na msitu kwapani kwa kuwa pesa zimemzidi.

 

Amber Lulu ameliambia Gazeti l a Ijumaa kuwa, kwa sasa pesa zimemtembelea kiasi cha kumfanya awe bize na kukosa muda wa kujifanyia usafi wa kunyoa makwapa.

 

“Unaweza kumkuta mtu ana pesa nyingi, ukasikia hebu muangalie hajipendi wala hajui kuvaa, hicho ndicho kinachonitokea, nimejikuta nimelisahau hata kwapa langu na sehemu nyingine kutokana na kuwa bize na mambo ya pesa,” amesema Amber Lulu.

Stori: Imelda Mtema, Dar

Toa comment