AMBER LULU, ASIYEFUNZWA NA MAMAYE…… !

Lulu Eugene ‘Amber Lulu

SIZUNGUMZII kuhusu mitusi ambayo mwanadada Lulu Eugene ‘Amber Lulu’ alikuwa akivurumishiana na mpenzi wake wa zamani, David Genzi almaarufu kama Young Dee, hapana! Amber Lulu ambaye alipata umaarufu akiwa kama video queen kabla ya baadaye kujiongeza na kuanza kuimba, amelizua jambo. 

 

Safari hii msanii huyu aliyewahi kuimba wimbo uitwao Jini Kisirani, ametia aibu mbele ya viongozi wa dini na kila mmoja bado haamini kama kweli kuna wanawake ambao wamekosa maadili kama alivyo Amber Lulu.

 

Iko hivi, siku kadhaa zilizopita, Amber Lulu na wasanii wengine kadhaa malegendari, wakiwemo Fareed Kubanda ‘Fid Q’, Juma Mchopanga ‘Jay Moe’ Mensen Selekta na wengine kadhaa, pamoja na Amber Lulu walisafiri na kwenda jijini Mwanza kwa ajili ya shoo ya muziki.

 

Baada ya shoo, walitakiwa kurudi jijini Dar es Salaam kwa ndege na hapo ndipo vituko vilipoanza. Wakati anawasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwanza pamoja na wasanii wenzake, Amber Lulu alikuwa tayari ameutwika kisawasawa kiasi cha kufanya mambo ya aibu mbele za watu.

 

Yote tisa, kumi ni baada ya kupanda kwenye ndege. Kabla hata safari haijaanza, Amber Lulu aliliamsha dude ndani ya ndege, akawa anaongea hovyohovyo, mara akwaruzane na abiria wenzake na kila baada ya maneno mawili au matatu, alikuwa akivurumisha ‘mitusi’ bila kujali kwamba alikuwa ndani ya usafiri wa umma, tena kukiwa na abiria wa aina tofautitofauti.

 

Kibaya zaidi, ndani ya ndege hiyohiyo ndimo walipokuwemo viongozi wa juu kabisa wa Baraza la Waislam Tanzania, akiwemo Mufti wa Tanzania, Abubakary Zuberi na Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum na mashehe wengine wanaoheshimika.

 

 

Sasa hebu vuta picha, jinsi Amber Lulu alivyo mwepesi wa kutoa lugha chafu kinywani mwake, ameutwika kisawasawa halafu anafanya yake bila kujali chochote! Ilikuwa ni aibu kwelikweli, watu wengine walikuwa wanatamani ndege iwe daladala, kwamba unaweza kushuka muda huohuo na kupanda nyingine lakini hilo halikuwezekana.

 

Hakuishia tu kutukana, kuna wakati alienda maliwatoni ndani ya ndege humohumo, ila kwa sababu ya kuzidiwa na ulabu, alisahau kujisitiri vizuri baada ya kumaliza haja zake.

 

Ilibidi mpaka uongozi wa juu uingilie kati na ikatangazwa ndani ya ndege hiyo kwamba kama kuna mtu hayupo tayari kwa safari, basi ashuke, ndiyo kidogo akaufyata. Sasa unajaribu kujiuliza, huyu binti amelelewa katika mazingira ya aina gani mpaka awe ‘fyatu’ kiasi hiki?

 

Amber Lulu, kwenu hakuna wakubwa? Hata kama wewe unaamini katika dini nyingine, huwezi kuogopa kufanya mambo yasiyofaa mbele za viongozi wakubwa wa dini ngazi ya taifa? Kilichokuwa kinakusumbua ni ushamba wa kupanda ndege au ulimbukeni wa pombe za bure?

 

Unataka watu wakufahamu kupitia kazi zako au vituko vyako? Kujichetua na kujitoa fahamu hazijawahi kuwa sifa zinazompendeza mtoto wa kike, kiumri wewe bado ni mdogo sana lakini kwa huu mwendo unaoenda nao, sidhani kama utafika popote zaidi ya kutoa vinyimbo viwili vitatu na kupotea kwenye ramani ya muziki.

 

Ukishakuwa msanii, tayari unakuwa ni ‘brand’ ambaye kila kitu chako lazima kiwe katika sura nzuri, kuanzia tabia, kauli, mwonekano na hata jinsi unavyoishi na watu wengine. Umaarufu hautafutwi hivyo, fanya kazi kila mtu atakutambua na kukuheshimu.

Loading...


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment