Amber Lulu Atamani Kuwa Kama Wema


MREMBO mwingine kunako Bongo Flevani, Lulu Eugen ‘Amber Lulu’ anachukizwa na ubonge nyanya alioupata ghafla na sasa anatamani kuwa mwembamba kama mwigizaji Wema Isaac Sepetu.

 

Amber ameiambia OVER ZE WEEKEND kwamba, kuwa na mwili mwembamba ni raha kwa sababu unakuwa na uwezo wa kufanya kazi yoyote kwa urahisi zaidi tofauti na ukiwa bonge.

 

“Kweli kabisa, natamani kurudi enzi zangu, nilikuwa na mwili mwembamba, mzuri na mwepesi, lakini siku hizi najiona mzito,” amesema Amber anayekimbiza na ngoma yake mpya ya Walete aliyomshirikisha Kusah.

STORI: MEMORISE RICHARD

Toa comment