Amber Lulu: Najilaumu Kuunadi Mwili Wangu Kwenye Mitandao
Lulu Euggen almaarufu Amber Lulu; ni muuza nyago (video vixen) na ni msanii wa Bongo Fleva anayefanya vizuri ambaye anafunguka kuwa, kipindi cha kukaa utupu ili mtu upate umaarufu kimepita badala yake hivi sasa ni kupiga kazi tu ili maisha yaendelee.
Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Amber Lulu anasema kuwa, kwa upande mwingine hata yeye alikuwa akifanya makosa kuacha mwili wake wazi, lakini sasa akili yake imepanuka na ana mtoto anayemtegemea kwa kila kitu hivyo hataki kusikia mambo hayo tena kwenye maisha yake.
“Kukaa uchi na kujiachia sehemu kubwa ya mwili kwa sasa ni ushamba na vitu hivyo vimepitwa na wakati kwa sababu hata mimi najilaumu sana kuunadi mwili.
“Mimi ni mama sasa na najitambua na ninataka mtoto wangu aige mfano mzuri kutoka kwangu,” anasema Amber Lulu anayetamba na wimbo wake wa Nimeachika.
Kabla ya kuwa mama na kujitambua, Amber Lulu alisifika kwa kuvaa na kujiachia nusu utupu, lakini sasa akili imemkaa sawa.
Stori; Imelda Mtema, Dar