The House of Favourite Newspapers

AMBER LULU: NATAMANI SANA MTOTO ILA RAMANI HAZISOMEKI

Lulu Euggen ‘Amber Lulu’

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Lulu Euggen ‘Amber Lulu’ amesema amekuwa akitamani na yeye aitwe mama kama ilivyo kwa wenzake lakini namna ya kumpata mtoto ndiyo anashindwa kujua kwani ‘ramani haisomeki’.  

 

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Amber alisema kuwa iwapo atapata mwanaume wa kuishi naye ambaye hana longolongo, ataanzisha naye familia lakini kwa sasa maisha yake ya kimapenzi hayaelewielewi.

 

“Siyo kwamba sipendi watoto jamani lakini naona bado ramani haijasomeka kabisa maana siyo nazaa halafu hata ‘pampers’ ya kumvalisha mtoto nakosa, kitu hicho sikipendi kabisa, bado naangalia kwanza, kwani kuzaa sio fasheni,” alisema Amber Lulu.

STORI: Imelda Mtema, Dar

Usichokijua kuhusu Mpenzi Mpya wa DIAMOND

Comments are closed.