The House of Favourite Newspapers

AMBER RUTTY Ajisalimisha Polisi na Bwana’ke – Video

MUUZA nyago kwenye video za Bongo Fleva, Amber Rutty amejisalimisha katika Kituo cha Polisi Mbagala, wilayani Temeke kutii maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kufuatia video kusambaa mitandaoni zikimwonyesha msanii huyo akifanya ngono na bwana yake kinyume cha maumbile. 

 

Baada ya video hizo kusambaa na kuzua maswali na taharuki miongoni mwa Watanzania, Makonda aliagiza msanii huyo ajisalimishe kwenye kituo chochote cha polisi kilicho karibu naye kabla ya jana saa 12 jioni na ujumbe wake ataukuta kituoni.

 

Tukio hili limejili ikiwa ni mwezi mmoja umepita tangu video za msanii huyo kuonekana akifanya mapenzi na wasanii wa Bongo Fleva wanaounda kundi la Mabantu, Twaa na Muu, ambapo Global TV ilimtafuta na kumbananisha kuhusu tukio hilo la ajabu, alikiri na kuomba radhi kwa Watanzania waliokwazwa.

 

Kwa tukio la hivi karibuni, Amber Rutty amesema upuuzi huo aliufanya zamani na video hizo zilikuwa kwenye simu ya bwana yake huyo ambaye amedai simu hiyo iliibiwa hivyo wezi wa simu ndiyo walisambaza video hizo.

 

Aidha, Amber Rutty amesema hahusiki na kusambaza video hizo mitandaoni huku akiliomba jeshi la polisi na mamlaka za uchunguzi kufuatilia kubaini aliyesambaza video hizo kisha kumchukulia hatua.

VIDEO: TAZAMA ALIVYOTINGA POLISI

Comments are closed.