The House of Favourite Newspapers

AMBER RUTTY ATINGA KISUTU NA MCHUNGAJI

Msanii Nascat Abubakar ‘Amber Rutty’ na mpenzi wake Said Mtopari, wamefika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo, Desemba 10, 2018 kwa ajili ya kusikiliza kesi yao wakiambatana na Mchungaji Daudi Mashimo ambaye aliwawekea dhamana mahakamani hapo.

Mbali na Amber Rutty na Mtopali mshtakiwa wa tatu katika kesi hiyo ni James Charles maarufu ‘James Delicious’ tayari yupo nje kwa dhamana. Washtakiwa hao wanakabiliwa na makosa manne. Katika kosa la kwanza ni la kufanya mapenzi kinyume na maumbile ambalo linamkabili Amber Rutty, anadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Oktoba 25, 2018 ambapo alimruhusu Mtopali kumuingilia kinyume na maumbile, kosa ambalo amelikana.

Katika shtaka la kufanya mapenzi kinyume na maumbile, linalomkabili Mtopali anadaiwa kati ama baada ya Oktoba 25, 2018 jijini Dar es Salaam alifanya mapenzi na Amber Rutty kinyume na maumbile. Kosa la tatu la kuchapisha video ama picha za ngono, linalomkabili James Charles ama James Delicious inadaiwa kati ya Oktoba 25, 2018, Charles alisambaza video za ngono kupitia makundi ya WhatsApp.

Kosa la nne ambalo ni kusababisha kusambaa picha za ngono linamkabili Amber Rutty na Mtopali wakidaiwa kati Oktoba 25, 2018 walisambaza picha za ngono kupitia makundi ya Whatsapp, jambo ambalo walilikana.

 

Hata hivyo, kesi hiyo imeahirishwa hadi January 10, 2019 itakapokuja kutajwa tena kutokana na upelelezi kutokamilika.

Comments are closed.