Amber Rutty, Mumewe, James Delicious Jela Miaka 5

MSANII Rutyfiya Abubakary maarufu kama ‘Amber Rutty’ na mpenzi wake, Said Bakary, pamoja na mtuhumiwa mwenzao, James Charles ‘James Delicious’, wamehukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kulipa faini ya ya Tsh milioni 11 ama kutumikia kifungo cha miaka mitano jela baada ya kupatikana na hatia katika makosa matatu likiwemo kosa la kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

 

“Nimezingatia hoja za pande zote mbili na athari za makosa haya, ni kweli washitakiwa wote vijana na wanategemewa, nimeona mshitakiwa wa kwanza anajutia, kutokana na mazingira ya kesi hii adhabu yake ni miaka 30 kila kosa ambapo nikiwafunga mtapotea kabisa,” amesema Hakimu Mkazi Mfawidhi Godfrey Isaya.

 

“Hivyo kwa mazingira mliyoyasema na lengo la adhabu ni kujirudi, mshitakiwa wa kwanza utalipa milioni tatu ama jela miaka mitano (Amber Rutty), mshitakiwa wa pili utalipa faini ya milioni tatu ama jela miaka mitano (Said Bakary ) na mshitakiwa wa tatu faini milioni tano ama jela miaka mitano (James Charles) na adhabu zitaenda sambamba,” ameongeza.

 

Hata hivyo, washtakiwa hao, ambao walikuwa wakikabiliwa pia na makosa ya kusambaza video zenye maudhui ya ngono mitandaoni, wameshindwa kulipa faini hiyo na hivyo wamepelekwa gerezani.

 

Toa comment