Kartra

Ambundo Achochea Moto Yanga

DICKSON Ambundo, ingizo jipya ndani ya Yanga ameweka wazi kuwa ni furaha kwake kuweza kusaini ndani ya timu hiyo hivyo atapambana kwa ajili ya kutimiza malengo.

 

Aliibuka ndani ya Yanga akitokea Dodoma Jiji na taarifa zinaeleza kuwa dili lake ni la milioni 50 huku mkataba wake ukiwa ni wa miaka miwili.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Ambundo alisema kuwa ni furaha kwake kusaini katika timu hiyo na anaamini atafanya vizuri kwa kushirikiana na wengine.

“Nimeshakamilisha masuala ya usajili, hivyo kwangu ni furaha na ninaona kwamba ni wakati mzuri kwa ajili ya timu na inawezekana kwa ushirikiano ambao tutaonyesha,” alisema Ambundo.

Kabla ya kupewa dili jipya Ambundo alifanya majaribio kwa kucheza mechi za Kombe la Kagame na alicheza mechi tatu na timu hiyo iliishia hatua ya makundi.


Toa comment