The House of Favourite Newspapers

AMEUMBUKA: KIGOGO POLISI ANASWA NA KIBINTI KITANDANI – VIDEO

MOROGORO: Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni na kama ni kuumbuka, basi huku ndiko kuumbuka kwenyewe, Risasi Mchanganyiko lina habari nzito!  

Kigogo wa Jeshi la Polisi nchini ambaye alikuwa Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani wa Mkoa (RTO) kabla ya kustaafu, Mashaka Mdachi amejikuta akipatwa na fedheha ya mwaka baada ya kunaswa ‘live’ kitandani kwake akiwa na ‘kabinti kadogo’.

 

NI DENTI WA MSINGI

Binti aliyekutwa naye chumbani ni denti wa shule ya msingi anayesoma darasa la tano (jina lake na shule vinahifadhiwa kwa kuzingatia maadili).

Tukio hilo lililowaacha midomo wazi watu wengi lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita, majira ya asubuhi kwenye moja ya vyumba vilivyo kwenye nyumba namba 691 inayomilikiwa na afisa huyo wa zamani wa Jeshi la Polisi iliyopo Mtaa wa Area- Five Kata ya Kichangani mjini hapa.

 

TUJIUNGE NA MWANDISHI WETU

Mwandishi wetu, akiwa kwenye majukumu yake ya kila siku, alipenyezewa taarifa za tukio hilo na kutinga fasta kisha kushuhudia askari kanzu zaidi ya sita waliokuwa na silaha nzito ‘wakimtaiti’ bosi wao huyo mstaafu.

 

Kabla ya yote mwandishi wetu alitaka kujua tatizo ni nini ndipo akaelezwa na askari hao kuwa kigogo huyo mwenye umri wa zaidi ya miaka 50 alikutwa live chumbani kwake akiwa kitandani na mtoto huyo mwenye umri wa miaka 11 ambaye ni sawa na mjukuu wake.

Kama kawaida, baada ya kuhakikishiwa kuwepo kwa tukio hilo, mwandishi wetu alipiga picha kisha akahamia kwenye kipengele cha pili cha mahojiano na watu mbalimbali juu ya kile kilichotokea.

AFISA USTAWI WA JAMII

Wa kwanza kuhojiwa kwenye tukio hilo ni Afisa Ustawi wa Jamii Kata ya Kichangani, Jamila Malima ambaye alikuwa na haya ya kusema;

“Wiki moja iliyopita mama mzazi wa mtoto huyu alifika ofisini kwetu akiwa ameambatana na walimu wa mtoto huyu. “Mama wa mtoto huyu alidai kwamba kwa siku za hivi karibuni alimshuhudia mwanaye akiwa na mabadiliko mwilini hivyo akaamua kumchunguza na kubaini ameharibika sehemu zake za siri.

 

“Alisema alipombana mwanaye alidai huwa anakuja kwa mzee huyu kufanya naye mambo ambayo yamemsababishia kuharibika. “Kwa upande wa walimu walipokea taarifa hizo kwa mzazi wa mtoto huyo na wao kama walimu walimbana ndipo akamtaja mzee huyo.

“Mtoto huyo aliwaambia walimu wake kwamba huwa haendi peke yake kwani kuna wenzake watatu. “Hivyo walimu na mzazi huyo waliamua kuja kwenye ofisi zetu kutoa taarifa na mimi ili kujiridhisha niliamua kutega mtego.

 

“Baada ya mtoto huyu kutoka shuleni, kama kawaida tulimwambia aende kwa mzee huyo kama anavyoendaga na sisi tukiwa jirani ya nyumba hii. “Kweli alipofika alikaribishwa ndani na dada wa kazi na mzee alipopewa taarifa alimtaka mtoto huyu aondoke kwa kuwa siku hiyo alitembelewa na wageni na asingependa wajue kinachoendelea hivyo akamwamuru aje leo.

“Sasa mtoto huyo alipofika hapa leo na sisi tulikuwa tunamfuatilia ndipo mzee huyu akamuingiza chumbani kwake. “Nilipoona hivyo ndipo nikaamini na kuwaita Polisi ambao wamemkamata live akiwa kitandani na binti huyu.”

 

MZEE HANA MKE?

Alipoulizwa kama mzee huyo hana mke, afisa huyo wa ustawi wa jamii alijibu: “Nasikia mkewe alimkimbia, lakini ukweli wa jambo hilo muulize mwenyekiti wa mtaa huu.”

 

MWENYEKITI WA MTAA

Akizungumzia ishu hiyo, mwenyekiti wa mtaa huo, Twaibu Dowile, kwanza alithibitisha kutokea kwa tukio hilo baya. Alisema: “Huyu mzee ni Afisa wa Jeshi la Polisi mstaafu aliyekuwa na cheo cha RTO (Regional Traffic Officer).

“Awali alikuwa na mke, lakini mkewe aliondoka sijui ni kwa sababu gani. “Lakini baadhi ya watu wanadai mzee huyu anasumbuliwa na ugonjwa fulani ambao kama unavyoona haoni vizuri.

 

MTOTO VIPI?

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko katika mahojiano maalum baada ya kuokolewa asifanyiwe ‘unyambilisi’ huo, mtoto huyo alidai kwamba mzee huyo amekuwa akimpa shilingi elfu mbili hadi elfu tano na ‘kumchezea’.

Alipotakiwa kuelezea mazingira aliyokutana na mzee huyo hadi kufikia hatua ya kukubali kuchezewa mwili wake na mzee ambaye ni sawa na babu yake, alijibu: “Kama unavyoona nikitoka shuleni ninapita njia ambayo ipo jirani kabisa na nyumba ya huyu mzee. “Sasa wakati tukitoka shule huwa anatuita, tunacheza naye nje, tukiondoka anatupa pesa.

 

“Hivi karibuni amekuwa haoni vizuri hivyo kila tukija tunaambiwa yuko ndani. “Huyu dada wa kazi anatukaribisha, tukifika ndani ndiyo anaanza kutupapasa kisha kutuvua nguo na kutuchezea. “Akishafanya hivyo huwa anatupatia pesa na kutuambia tuje tena kesho yake.”

 

MAMA MZAZI SASA

Naye mama wa mtoto ambaye naye alikuwepo eneo la tukio alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo, muda wote alikuwa bize kuzungumza na mumewe na ndugu zake hadi alipopanda kwenye difenda la Polisi na kwenda kituoni.

MTUHUMIWA ANASEMAJE?

Kwa upande wake mzee huyo alipohojiwa alikuwa akimjibu mwandishi wetu kwa mkato kwamba tukio hilo ni la kupangwa.

Alipotakiwa kufafanua juu ya tukio hilo kupangwa na kwa nini alikubali kujifungia chumbani na mtoto huyo hakuwa na majibu. Kigogo huyo wa Polisi ilielezwa kuwa alifanya kazi mkoani hapa kabla ya kuhamishiwa Mtwara ambako alifanya kazi hadi alipostaafu.

 

UCHUNGUZI WA POLISI

Mmoja wa polisi waliomkamata mzee huyo aliyejitambulisha kwa jina la Afande Mwajabu alisema kuwa, baada ya hapo kitakachofuata ni kufanya uchunguzi ambapo mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara moja.

“Hapa tunakwenda mahabusu kisha uchunguzi utafanyika kwa ajili ya kufikishwa mahakamani,” alisema Afande Mwajabu. Jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa hazikuzaa matunda. Hata hivyo gazeti hili linafuatilia kwa karibu tukio hili ili kujua mwisho wake.

Stori: DUNSTAN SHEKIDELE, RISASI MCHANGANYIKO

Comments are closed.