The House of Favourite Newspapers

Amfumania mume, achoma nyumba!

1

afumaniwa (4) Monika akiwa amezimia.

Waandishi wetu, Amani

Dar es Salaam: Mapenzi uchizi! Hii ndiyo kauli pekee unayoweza kuitumia baada ya mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Monika, mkazi wa Tabata-Senene jijini Dar, kudaiwa kumfumania mumewe na mchepuko ndani kwake kisha kuchoma moto nyumba kabla ya kuzimia.

afumaniwa (3)Nyumba ilivyochomwa moto.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo lililojaza umati, sekeseke hilo lilijiri wiki iliyopita, mishale ya saa 5:00 asubuhi nyumbani kwa wanandoa hao maeneo hayo ambapo mwanamke huyo hakuwepo nyumbani hivyo aliporudi ndipo akaanzisha timbwili, akidai kumkuta mumewe ndani na mchepuko.

afumaniwa (2)“Unaambiwa baada ya Monika kurudi nyumbani na kumfuma mumewe ‘akimalizana’ na mchepuko, palikuwa hapatoshi.

“Monika aliangusha timbwili la aina yake lakini yule mchepuko alifanikiwa kutoka nduki.

afumaniwa (5)“Kutokana na hasira, Monika alijifungia ndani, akamwagia nyumba mafuta ya taa, akawasha moto akitaka kujitoa uhai.

“Tunashukuru Mungu, askari wa zima moto walifika na kufanya jitihada za kumuokoa akiwa bado hajaungua la sivyo sasa hivi tungekuwa tunazungumza mengine.

afumaniwa (6)“Kilichomsaidia Monika, baada ya kuona moto umepamba, akili ilimrudi na kuanza harakati za kutaka kutoka ili ajiokoe huku mumewe akihaha kwa fedheha aliyoipata na hasara ya kuchomewa nyumba yake.

“Hata hivyo, Monika alitolewa ndani akiwa amepoteza fahamu,” alisimulia mmoja wa mashuhuda hao.

Amani lilifika eneo la tukio na kuzungumza na majirani ambao walikiri kutokea kwa mkasa huo ambao kwao ni wa kihistoria na kulaani kitendo hicho kisijirudie mtaani kwao.

afumaniwa (1)“Hata kama walikuwa na mgogoro, haikupaswa kufanyiana ukatili huo maana kila mmoja ana makosa, maisha haya yalivyo magumu kuchoma nyumba si sawa hata kidogo, pia usaliti upo ila huo umevuka kiwango,” alisema mmoja wa majirani hao kwa sharti la kutotajwa gazetini.

Ili kuweka sawa mzani wa habari hiyo, gazeti hili lilizungumza na mwanaume huyo ambaye hakuwa tayari kutoa ushirikiano kwa madai kuwa suala la kuchomewa moto nyumba yake lipo kwa mwanasheria wake hivyo hawezi kulizungumzia.

Juhudi za kumpata mkewe ziligonga mwamba lakini alipopatikana mjumbe wa eneo hilo, Joseph Salim alieleza namna alivyosikitishwa na tukio hilo huku akiwalaumu mke na mume kutokana na mwanamke kuchukua sheria mkononi na mwanaume kuingiza mchepuko nyumbani anapoishi na mkewe.

Hata hivyo, kwa mujibu wa mjumbe huyo, tukio hilo halikufikishwa polisi kwa maelezo kuwa watamalizana wenyewe (mke na mume).

Waandishi: Mayasa Mariwata na Issa Mnally.

1 Comment
  1. annie says

    LOL MAJARIBU MAKUBWA, NA HUYO MWANAUME NI MUUAJI, KUMLETA MCHEPUKO HADI NDANI! NI KOSA KUBWA , SASA NYUMBA HANA ILA MCHEPUKO ANADUNDA. kHAA!

Leave A Reply