The House of Favourite Newspapers

Amina Vikoba Atangaza Kuachana na Mume Wake, Apata Hati ya Talaka

0
Msanii maarufu wa maigizo nchini, Amina Ahmed ‘Amina Vikoba’.

Msanii maarufu wa maigizo nchini, Amina Ahmed ‘Amina Vikoba’ ambaye amekuwa kipenzi cha wengi kupitia tamthilia mbalimbali, amefunguka kuhusu maisha yake ya ndoa. Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram, Amina amethibitisha kuwa yeye na mume wake wameachana rasmi baada ya kupata hati ya talaka.

Katika ujumbe wake, Amina alieleza kwamba ingawa hatua hiyo haikuwa rahisi, imekuwa muhimu kwa ustawi wa pande zote mbili. Aliongeza kuwa maisha ya ndoa yana changamoto zake, na wakati mwingine ni muhimu kuchukua maamuzi magumu ili kuendelea mbele.

Mashabiki wake wengi walionekana kushangazwa na taarifa hiyo, huku wakimpa moyo na kumtakia kila la heri katika maisha yake mapya. “Ninyi mashabiki wangu mmekuwa nguzo yangu kwa muda mrefu, na nawaahidi nitazidi kufanya kazi nzuri kuwapa burudani bora zaidi,” alisema Amina kupitia ujumbe wake.

“Bismillah Alhamdulilah Namshukuru mungu kwa mwaka mwingine na maisha mengine mapya 🙏 mimi Amina Ahmed rasmi sio mke wa mtu
Shetan anapotupa majaribu Basi M/mungu hutuonesha njia ya kushinda vita hiyo
Binafsi ninafuraha sana kwasababu nmepata aman na utulivu wa moyo wangu jamon ndoa zinachangamoto sana tunavumilia sana na inafika hatua tunachoka
Kama isemavyo dini yangu pendwa ya kiislam mnaoana kwa amani na ikifikia hatua mmeshindwana Basi iwe kwa amani 🙏
Napenda kumshukuru mwenyez mungu kwa maisha yangu yaliyopita ya ndoa na ninapenda kumuomba M/mungu anisimamie na anifanyie wepesi kweny maisha yangu mapya 🙏 AMIN INSHAALLAH

Kubwa la maadui
Siwa Binti kikala
Amina VIKOBA 
Asanteni mashabiki zenu endeleeni kuni support na mm nawaahidi sitowaangusha kwa uwezo wa Allah ❤️ Nawapenda sana” Amina Vikoba

NYUMBA ya KIFAHARI ya PARIS HILTON YATEKETEA kwa MOTO MKUBWA UNAOWAKA MAREKANI – MWENYEWE ASHUHUDIA

Leave A Reply