Amini: Bila Malipo Siandikii Mtu Wimbo

 

MWANAMUZIKI anayeta­mba na Ngoma ya Yamoyoni, Amini Mwinyimkuu ameeleza kuwa kutokana na hali ya maisha kuzidi kuwa ngumu kwa sasa hana mpango wa kumwandikia mwanamuziki yeyote wim­bo bila malipo.

 

Akistorisha na Mikito Nusunusu, Amini alisema ni muda mrefu amekuwa akiwaandi­kia wanamuziki wenzake nyimbo bure lakini kwa sasa hawezi kufanya hivyo tena kwa kuwa maisha yamebadilika sana na yanazidi kubadilika kila kukicha hivyo vya bure tena kwake hakuna.

 

“Kiukweli bila mpunga simwandikii mtu wimbo maana nimefanya kazi hiyo bure kwa muda mrefu sana hivyo kwa sasa hata akiwa hana shoo fedha atakazopata kwa ku­waandikia watu nyimbo zitamsaidia katika kuendesha maisha,” alisema Amini.

Stamina, Darassa Kulipeleka Jiji Dar Live Sikukuu ya Idd Mosi


Loading...

Toa comment