The House of Favourite Newspapers

Amini: Mimi na Linah, Ngumu Kutengana!

0

MWANAMUZIKI Amini Mwinyimkuu, ni mmoja kati ya wanamuziki walioibuliwa kutoka kwenye Jumba la Vipaji Tanzania (THT) na kuweza kufanya vizuri sana kwenye anga la Bongo Fleva.

 

Amini ambaye alipotea kidogo, kisha hivi sasa ameibuka upya, amefunguka vitu vingi kuhusu muziki na maisha yake binafsi:
Amini kuna kipindi cha nyuma uliibuka na nyimbo kali mbalimbali, lakini baada ya muda ulipotea tena kabisa na watu walikuwa wanajiuliza uko wapi?

 

Amini: Mimi kupotea kwangu sio kwamba nilikuwa nimebweteka, ukweli nilikuwa siingii studio, bali kuna kazi za kijamii nilikuwa nafanya kama za kwenda vijijini na ni mbali sana, hivyo ni ngumu kutoa ngoma.

 

Amani: Sasa kukaa kimya huoni kama unaweza kupoteza mashabiki wako?

Amani: Unajua mtu mwingine anaweza kufi kiri hivyo, lakini ukweli ni kwamba msanii wa kweli atabaki tu hata asipoimba muda gani, maana si vyema kuingia studio tu na kukurupuka.

Amani: Wakati ulipopotea kwenye anga la muziki, ulikuwa unawezaje kuendesha maisha yako ya kila siku maana najua ili maisha yasonge ni kutoa nyimbo na kupata shoo.

 

Amini: Wakati nikihangaika na kazi za kijamii, nilikuwa napata hela ya kukidhi mahitaji yangu wala kulikuwa hakuna shida yoyote ile.
Amani: Una muda mrefu kama miaka saba hukuwahi kufanya nyimbo ya pamoja na Linah baada ya kuachia ile ya mtima wangu ilikuwa ni sababu ya kuogopa mwanaume aliye naye na wewe mke uliyeoa au?

 

Amini: Kwanza kabisa watu wajue kwamba, mwanaume aliyemuoa Linah anajua alimtoa kwangu na mke wangu hivyohivyo alijua alinitoa kwa Linah, hivyo hakuna ambaye angezuia tusiimbe pamoja.

 

Amani: Inasemekana kutengana kwa Linah na mwenzie na wewe kuachana na mwenza wako, ni kutoka na visa vyenu mlivyovipanga, je kuna ukweli?

 

Amini: Hapana, yaani ni tofauti kabisa, watu wanasema hivyo lakini hawajui undani wowote, yaani sisi wawili kila mmoja
ametengana na mwenziye kwa sababu tofauti kabisana ukichunguza kila mmoja alikuwa na tukio lake.
Amani: Kwa hiyo ni sababu gani ilikufanya ukaacha na mkeo?

 

Amini: Hiyo ni mambo binafsi siwezi weka hadharani na kingine ikiandikwa mtu anaweza kukata kipande cha gazeti akabandika kwake, siku mtoto wangu akikua na akasoma itakuwa sio vizuri, nitamuharibu kisaikolojia.

Amani: Kwa hiyo, sasa umeamua kurudiana na Linah kabisa?

Amini: Unajua Linah hata ambavyo tuliachanaga hakuna mtu aliyegomba na mwenzake kabisa na kingine si unajua true love never die, amerudi na amenasa ingawa atakuwa na mahusiano yake mengine.
Amani: Hivi mlibahatika kupata mtoto wewe na mkeo?

Amini: Ndiyo tena dume la mbegu.
Amani: Mara nyingi mlikuwa na ukaribu sana na Barnaba (Elias) lakini sasa hivi sijawahi kuwaona pamoja tatizo nini?

Amini: Tupo tena vizuri sana sema kila mtu anayasaka maisha yake na kutafuta mbinu za kusonga mbele, lakini tunakutana kuzungumza mengi ya maendeleo.
Amani: Haya shukrani
Amini: Asante.

Leave A Reply