The House of Favourite Newspapers

Amtosa Mumewe Ulaya, Achukuliwa na Kiserengeti cha Gambia

0
Mama mwenye watoto tisa Heidi Hepworth (44) akiwa na mpenzi wake wa sasa Mamadou Jallow.

 

MWANAUME mmoja mkazi wa Uingereza Andy Hepworth, amesimulia kwa huzuni jinsi mkewe Heidi Hepworth (44) alivyomtosa, akamwachia watoto tisa na hivi sasa anajirusha na kivulana cha kutoka Gambia, Afrika.

 

Mwanamke huyo anaishi na kijana huyo anayejulikana kama Mamadou Jallow (30) baada ya kufahamiana kupitia Mtandao wa Facebook ambapo aliamua kumfuata hukohuko Gambia na mpaka sasa anaishi naye huko.
Jinsi alivyokolewa na mapenzi hayo mapya, sasa Heidi anadai talaka na kusema kuwa amempata ampendaye zaidi.

…Enzi ya ndoa yao na mume wake Andy.

“Ni jambo la ajabu, alianza tabia ambazo sikuzifahamu. Alianza kwenda gym, akakodisha vitanda maalum vya kuotea jua kwenye fukwe, akaanza kujichora tattoo na kuvaa nguo za ajabu,” anasema Hepworth na kuongeza: “Amekuwa mtu wa ovyo. Mwanzoni alikuwa mama mwenye upendo na anayejua majukumu yake.

 

 

Hivi sasa ni kama shetani ameukamata mwili wake. Kijana aliyenaye ameivuruga akili yake ambapo na yeye anafuata kila kitu.” Heidi naye anasema: “Nimekutana na kijana mpya, jambo ambalo si la kushangaza.

…Akiwa na mume wake Andy.

Ndoa yetu imekuwa na matatizo kila mara. Tulijikuta hatuna uhusiano mwema,” Andy na Heidi walikutana mnamo miaka ya 1990 na wameishi kwa miaka 23 na kuzaa watoto tisa. Andy anasema: “Tulikutana akiwa na watoto watatu kutoka kwa mwanaume mwingine lakini niliwachukua kama wangu.

 

Afukuza ambapo mimi na yeye tulizaa watoto tisa.” Anaongeza kwamba alianza kuyaona mabadiliko kwa mkewe huyo tangu Machi mwaka huu baada ya kugundua majina ya marafiki wa kiume kutoka Afrika na Asia kwenye kompyuta yao ya nyumbani na alipomwuliza alikana.

Hivi sasa Heidi na Mamadou wanaishi jijini Banjul na mama huyo amekanusha kwamba anatumiwa na kijana huyo ili apate pasipoti ya kuingia Uingereza. “Hilo halipo kabisa, nimempenda, basi! Hakuna mwingine. Kuhusu watoto, bado nawakumbuka sana. Sidhani kama nitaondoka hapa, lakini watoto wangu bado nawakumbuka,” alisema Heidi.

Leave A Reply