The House of Favourite Newspapers

Amuua Kaka Yake kwa Sangoma Kisha Kujinyonga

WATU wawili wamefariki dunia Mkoani Morogoro baada ya mtu aliyedaiwa kuwa na ugonjwa wa akili kumuua ndugu yake na kisha naye  kujinyonga walipokuwa kwa mganga wa kienyeji kwaajili ya kupata matibabu.

 

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi wa Polisi Wilbrod Mtafungwa amesema kuwa tukio hilo limetokea Desemba 1, 2018 baada ya Lucian Kigolo (54) ambaye anamatatizo ya akili kumshambulia kaka yake Gerald Kigolo (60) kwa kumpiga na kitu kizito kichwani.

 

Aidha Kamanda Mtafungwa amesema baada ya kutenda tukio hilo, mtu huyo aliamua kujinyonga kwa kutumia kamba nyumbani kwa mganga wa kienyeji ambaye ametambulika kwa jina la Luka Paulo (50), ambapo katika tukio hilo Jeshi la Polisi linamshikilia mganga huyo.

KASALALI Ailipua Bodi ya Pamba Kwa Rais Magufuli

Comments are closed.