The House of Favourite Newspapers

Amuuwa Mmiliki wa Paka kwa Hasira

0

Unaambiwa huko Florida, jamaa mmoja anayejulikana kwa jina la Cliffton Bliss Jr (58) anashtakiwa kwa kosa la kumuuwa kwa risasi jirani yake James Taylor Jr (41) , ambaye alikuwa ni mmiliki wa paka.

Cliffton alifanya mauwaji hayo baada ya kukasirishwa na paka wa jirani huyo aliyeingia ndani ya chumba chake, taarifa za polisi zinasema Cliffton alishika bunduki yake na kutishia kumuuwa paka huyo lakini mmiliki wa paka akamsihi asifanye hivyo, na hapo ndipo Cliffton alipogeuza uwelekeo wa bunduki yake na kumpiga mmiliki wa paka na kupelekea kifo chake.

Uchunguzi bado unaendelea, lakini mshtakiwa alijitetea kwamba alitekeleza mauaji hayo baada ya kushambuliwa kwa matusi na mmiliki wa paka huyo!

Mtag rafiki yako asiyependa paka hapa tumjue!

Cc; @bakarimahundu

Leave A Reply